LEO TUTAJIFINZA somo la maisha ya maombi ili tufahamu kuishi maisha yale tunayo yaomba kila siku madhabahuni pa Bwana. Maombi ni nini maombi ni kuzungumza na yule mwenye kitu mfano maombi ya kazi; Huna kazi unawaomba wale wenye kazi, nk Ila leo tutazungumzia maombi ya imani kwa nini imani ? kwa sababu pasipo imani haiwezekani kumpendeza mungu. Mungu ni roho, haonekani kwa macho ya nyama yeye ni roho neno lake ni roho hivyo tunapaswa kuwa na imani; ( waebrania 11:6 ) Neno linasema hivi " Lakini pasipo imani haiwezekani kumpendeza, kwa maana mtu amwendeaye mungu lazima aamini kwamba yeye yuko, na kwamba huwapa thawabu wale wamtafutao " Tunapo funga macho na kuomba lazima tuamini yeye yuko, anaitaji kusikia maombi yetu anapenda kutuona tuna mtegemea yeye kwa kila jambo. Imani ndio macho yetu na mikono yetu ya kupokea majibu ya maombi yetu ( mathayo 21:22 ) Neno linasema hivi " Na yoyote mtakayoyaomba ktk sala mkiamini, mtapokea " Rafiki yangu; Je umejenga tamad...