__ Roho Mtakatifu anaweza kuutumia ukiwa uliopo ktk kumuongoza mtu __ Ukiwa ni ishara inayomjulisha mtu ya kuwa kuna jambo la kiroho linalohitaji matengenezo na mungu Hii ni kwa sababu kufuatana na ( Ezekiel 15:8 ) ( Yeremia 22:5 ) Ukiwa ni moja wapo ya adhabu ambazo mungu anaweza kuitoa kwa mtu au watu kutokusikia na kutokutii maagizo yake. __ Ikiwa mtu anasikia moyoni mwake ukiwa uliombatana na maombolezo na huzuni kwa wakati mmoja huo huo hiyo ni ishara ya ujumbe toka kwa Roho mtakatifu ya kuwa hali hiyo inahitaji maombi kwa mungu ili upewe maehekezo zaidi juu ya aina gani ya matengenezo ya kiroho yanayo hitajika ili hali hiyo iondoke. __ Hali hiyo ya ukiwa inaweza kuwa juu ya eneo au juu ya mtu au juu ya kundi la watu au juu ya wazo au juu ya tukio na tukaangalia utendaji wake juu wa roho na ukiwa juu ya eneo. Leo nataka tujifunze mambo kadhaa juu ya ujumbe ambao roho mtakatifu anaweza kuwa nao ukiwa unapokuwa juu ya mtu au juu ya kundi la watu roho mta...