__ Roho Mtakatifu anaweza kuutumia ukiwa uliopo ktk kumuongoza mtu
__ Ukiwa ni ishara inayomjulisha mtu ya kuwa kuna jambo la kiroho linalohitaji matengenezo na mungu
Hii ni kwa sababu kufuatana na ( Ezekiel 15:8 ) ( Yeremia 22:5 )
Ukiwa ni moja wapo ya adhabu ambazo mungu anaweza kuitoa kwa mtu au watu kutokusikia na kutokutii maagizo yake.
__ Ikiwa mtu anasikia moyoni mwake ukiwa uliombatana na maombolezo na huzuni kwa wakati mmoja huo huo hiyo ni ishara ya ujumbe toka kwa Roho mtakatifu ya kuwa hali hiyo inahitaji maombi kwa mungu ili upewe maehekezo zaidi juu ya aina gani ya matengenezo ya kiroho yanayo hitajika ili hali hiyo iondoke.
__ Hali hiyo ya ukiwa inaweza kuwa juu ya eneo au juu ya mtu au juu ya kundi la watu au juu ya wazo au juu ya tukio na tukaangalia utendaji wake juu wa roho na ukiwa juu ya eneo.
Leo nataka tujifunze mambo kadhaa juu ya ujumbe ambao roho mtakatifu anaweza kuwa nao ukiwa unapokuwa juu ya mtu au juu ya kundi la watu roho mtakatifu ktk mazingira yenye ukiwa juu ya mtu au juu ya kundi la watu anataka ufahamu mambo yafuatayo
Jambo la kwanza
Ukiwa ni hali halisi anayoipata mtu moyoni mwake, ili kumjulisha ya kuwa kuna jambo linalomhusu mtu huyo linalohitaji matengenezo ya kiroho.
Biblia inasema : Basi tamari akakaa halinya ukiwa nyumbani mwa nduguye Absalomu ( 2samweli 13:20 )
Hali hii ilimpata tamari baada ya kubakwa na Amnoni na Amnoni kukataa kumwoa kufuatana na ( kumbuku ya torati 22:23,27 )
Msichana au mwanamke anapobakwa na kukaa kimya naye anakuwa na kosa mbele za mungu linalohitaji matengenezo ya kiroho yaani toba
Jambo la 2:
Ukiwa unaweza kuwa kama vazi juu ya mtu Biblia inasema ktk ( EZekiel 7:27 ) ya kwamba na mkuu atavikwa ukiwa hii ikiwa na maana ya kuwa ukiwa unaweza kutembea au kwenda mahali ambapo mtu huyo anakwenda.
Hali hii ya ukiwa juu ya mtu ni tofauti na ile ya ukiwa juu ya eneo ukiwa ktk eneo unabaki kwenye eneo ukiwa ktk eneo unabaki kwenye eneo husika hata kama mtu aliyesababisha ukiwa ameondoka kwenye eneo hilo.
Ukiwa ukikaa juu ya mtu huwa unaondoka na kufuatana na mtu aliyenao kama vile nguo aliyovaa au vazi alilovaa.
Jambo la 3:
Ukiwa unatabia ya kuambukiza mtu aliye na ukiwa anaweza kuambukiza hali hiyo ya ukiwa kwa mtu aliye karibu naye.
Tamari alipovikwa hali ya ukiwa alienda nayo hadi nyumbani kwa ndugu yake aliyeitwa Absalomu.
Hali ile ya ukiwa iliyokuwa juu ya Tamari ya kubeba hasira na uchungu iliwapata au iliwavaa pia ndugu zake kama mfalme Daudi ( 2samweli 13:21 ) na vile vile Absalomu ( 2samweli 13:22 )
Hii ina maana pia ya kwamba ikiwa mkuu atavikwa ukiwa uwe na uhakika wale wanaomzunguka wataambukizwa hali hiyo ya ukiwa wa mkuu.
Baada ya muda si mrefu kumbuka: ukiwa ukiondolewa kwa mkuu au mkuu mwenye hali ya ukiwa akiondoka uwe na uhakika hali hiyo ya ukiwa itaondoka juu ya wale aliowaambukiza ukiwa wake.
Maoni
Chapisha Maoni