Kushirikiana Na Roho Mtakatifu Anapotumia Moto kukuongoza ili utembee kwenye mapenzi ya mungu
Biblia inafundisha ya kuwa wana wa mungu huwa wanaishi na wanatakiwa waishi kwa kuongozwa na roho mtakatifu ( warumi 8 : 14, 16, 17 ) Njia moja wapo anayotumia roho Mtakatifu kumwongoza mwana wa mungu, ni kwa kutumia moto wa mungu anaokuja nao ndani ya mtu anapoingia kukaa kwake
Biblia inasema juu ya yesu ya kuwa yeye atawabatiza kwa roho mtakatifu na kwa moto ( luka 3 : 16 ) na siku ya pentekoste, wakati wanafunzi wa kwanza wa yesu, walipokuwa wamekutanika pamoja kukuwatokea ndimi zilizogawanyika, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao wote wakajazwa roho mtakatifu ( matendo 2 : 3,4 )
Unaposoma na kutafakari jambo lililotokea siku hiyo ya pentekoste, utajua kuwa kuna uhusiano kati ya ndimi za moto juu ya kila mmoja wao na kule kujazwa roho mtakatifu kwa kila mmoja wao ni dhahiri ya kuwa roho mtakatifu anaingia ndani ya kila mwana wa mungu akiwa pia na moto wa mungu pamoja nao kazi moja wapo ya moto huo
Ni ili roho mtakatifu autumie kumwongoza mtu kwa kuuvuta moyo wake uwezo kuwa msikivu kwa kile ambacho mungu anamtaarifu kinachohusiana na mapenzi ya mungu kwake.
Mfano: Nguzo ya moto iliyowaongoza wana wa israeli wakiwa jangwani wakati wa usiku ( kutoka 13, 12, 22 ) kinapozungumza juu ya safari ya wana wa israeli ya kuelekea kaanani wakitokea misri utasoma hivi Bwana naye akawatangulia mchana ndani ya wingu mfano wa nguzo, ili awaongoze njia na usiku ndani ya moto mfano wa nguzo ili kuwapa nuru, wapate kusafiri mchana na usiku ile nguzo ya wingu haikuondoka mchana wala ile nguzo ya moto haikuondoka usiku mbele ya hao watu
Tunaona ya kwamba nguzo ya moto ilikuwa ni ishara ya kuwa, mungu alikuwa pamoja nao ili awaongoze njia na kuwapa nuru wapate kusafiri usiku, unaposoma ( yeremia 9:12 ) utaona ya kuwa mungu aliwaongoza wana wa isreli kwa nguzo ya moto usiku ili kuwapa mwanga ktk njia iliyowapasa kuiendea wazo hili unalipata pia unaposoma ( kumbukumbu 1:33 )
Je umewahi kujiuliza kwa nini mungu aliwaongoza kwa utaratibu tofauti mchana na kwa utaratibu mwingine usiku naamini ni ili tujue ya kuwa mungu anaongoza watu wake kwa namna tofauti kwa kufuatana na msimu wa maisha tofauti na usiku ni msimu tofauti
Roh mtakatifu anakuongoza wakati wa msimu wako wa mchana kwa utaratibu tofauti ukilinganisha na jinsi anavyokiuongoza wakati wa msimu wako wa usiku kipindi cha mtu cha usiku kiroho ni wakati ambapo anapitia kipindi kigumu kimaisha kiasi kwamba anaona amezungukwa na giza kimaisha, mtu akiendelea kwa muda mrefu kwenye kipindi kigumu kimaisha kama cha usiku au giza bila mungu kumpa uhakikisho ya kuwa yupo pamoja naye anaweza akafikiri ya kuwa mungu amemwacha
Ndio maana mtu anapopitia kipindi kigumu kimaisha mara kwa mara atasikia moyoni mwake uwako wa moto ambao utawaka kwa muda kadhaa kwa masaa au kwa siku kadhaa mfululizo hali ya uwako wa moto moyoni mwako wa namna hiyo ikikupata wakati wa msimu wako wa maisha yako unaofanana na usiku au giza ujue mungu anakupa uhakikisho ya kuwa yupo pamoja nawe katika Roho mtakatifu kukupa ili kukuonyesha njia uipasayo kuipitia ili uvuke hicho kipindi chako kilicho kigumu kimaisha mungu azidi kukubariki
Maoni
Chapisha Maoni