Roho Mtakatifu anataka ufahamu na ujue mambo gani ikiwa nakupa kukujulisha juu ya ukiwa kuwepo ktk eneo.
Biblia inasema ktk ( mwanzo 1:2 ) hivi nayo nchi ilikuwa ukiwa na roho ya mungu ikatulia juu ya uso wa maji kufuatana na neno nchi lilivyotumika hapa lina maana ya ardhi.
Hii ni kwa kuwa tafsiri nyingi za Biblia za uingereza zimetumia neno earth pamoja na kwamba ardhi hiyo ilikuwa chini ya maji au ilikuwa imefunikwa na maji.
Roho Mtakatifu aliweza kujua hali ya ukiwa iliyo kuwa kwenye ardhi ya eneo lile na tunaposoma ( Ezekiel 15:8 )
Tunajua ya kuwa ukiwa ni matokeo ya adhabu ya mungu mstari huu umeandikwa hivi nami nitaifanya nchi kuwa ukiwa kwa sababu wamekosa asema Bwana mungu mstari huu unatupa kujua jambo muhimu ya kwamba ukiwa unaweza ukakaa juu ya ardhi au ktk ardhi ya eneo hata kama eneo hilo la ardhi au ktk ardhi ya eneo hata kama eneo hilo la ardhi halina watu wakati huo
Je hali ya namna hii unapoisikia moyoni mwako UNAPOOMBEA eneo la ardhi unayotaka kununua kwa ajili ya kujenga nyumba au kuitumia kwa kilimo Roho Mtakatifu anataka kukupa ujumbe gani ??
Ikikutokea hali ya namna hiyo ujue Roho Mtakatifu anataka ufahamu ya kuwa
__ Eneo hilo lipo chini ya adhabu ya mungu
__ Kuna kosa lililofanywa na mtu au watu waliokaa au waliomiliki eneo hilo kabla yako
__ Kwamba kosa hilo linatakiwa lirekebishwe kwa toba kabla mtu mwingine hajaruhusiwa kuishi au kufanya kitu kwenye eneo hilo
__ Kwa sababu wewe ndiye unayetaka kufanya jambo kwenye ardhi hiyo na ufanikiwe inakubidi uwe mhusika pia wa kufanya toba hiyo kumbuka
__ Lengo la toba hiyo ni ili mungu asamehe na kuomba adhabu ya ukiwa juu ya ardhi hiyo hali ya adhabu ya ukiwa ndiyo mara nyingi ( si mara zote lakini mara nyingi ) imefanya maeneo mengi ya ardhi yawe tupu na yasiendelezwe hata kama ni maeneo mengi ya ardhi yawe tupu na yasiendelezwe hata kama ni maeneo mazuri kwa kuishi au kwa kulima au kwa kufanyia biashara
Taarifa hiyo ya Roho Mtakatifu haikuzuii kununua au kutumia au kuliendeleza hilo eneo Bali, Roho Mtakatifu anataka ujue adhabu hiyo ipo kwenye ardhi na ni vinzuri ushughulikie hiyo adhabu, ili mungu aiondoe.
Ndiyo maana ukiliombea hilo eneo utaona moyoni mwako unasikia kuomba kwa kuomboleza ( yeremia 4:25 )
Hali hiyo ya kuomboleza ni ishara toka kwa Roho Mtakatifu ya kuwa ombea hilo eneo wala usipuuzie na maombi yako yakipata majibu toka kwa Mungu utasikia moyoni mwako huko kuomboleza kumeisha moyoni mwako na ukiwa hutausikia moyoni mwako utakapokuwa unaombea au umekanyaga eneo hilo la ardhi
Jambo hili ni muhimu kwa kuwa adhabu ya ukiwa ktk ardhi ya eneo infanya eneo hilo
__ Lisikaliwe na watu ( Ezekiel 33:28 ) ( yeremia 51:29 )
__ Lisitembelewe na watu ( zakaria 7:14 )
__ Kitu kitakachofanyika hapo kisizae matunda au matokeo yaliyokusudiwa.
Maoni
Chapisha Maoni