Imezoeleka ukitaka kufurahia teknolojia za kisasa zaidi basi itakubadili kununua simu ghari zaidi, ila kwa simu ya jelly ni tofauti.
Utapata simu yenye mfumo wa 4G na Android 7.0 na kwa bei nafuu zaidi simu ya jelly inasifa ya kuitwa simu janja yenye umbo dogo zaidi duniani inayokuja pia na teknolojia ya mawasiliano ya 4G na pia toleo la kisasa na Android
Muonekano wa simu ya jelly
Simu hii ni simu nzuri tuu yenye uwezo wa kuzishinda simu nyingine nyingi za Android zinazouzwa kwa bei ya juu tuu na huku zikikosa sifa ya kuja na Android 7.0 na kwa uwezo wa 4G LTE.
Simu ya jelly inakuja ktk matoleo mawili jelly ya kawaida inayokuja na RAM ya GB1na diski uhifadhi wa GB 8.
Itauzwa kwa dola 109 za marekani, yaani takribani Tsh 220, 000/=
Pia kuna jelly pro yenye GB 2 ya RAM na diski uhifadhi wa GB 16 hii itaenda kwa dola 125 ( Takribani Tsh 250,000/=
Simu zote hizi kwa sasa zinapatikana kwa bei pungufu kwa watu wanaochangia matengezo ya mkupuo wa kwanza wa simu hizo.
Watu wanaotaka matoleo ya simu hizo kwa haraka zaidi wanaweza kufanya malipo kupitia mtandao wa kick starter ambapo simu zitaanza kutumwa duniani kote.
Sifa zake kwa uchache
__ Android 7.0 Nougat
__ 4G LTE
__ Laini mbili ( ukubwa wa nano )
1.IGHZ quad _ core processor
__ kioo mguso ( Touch screen / display ) cha incha 2.45 ( 240 ×432 resolution )
__ RAM GB 1 ( GB 2 kwa jelly pro )
GB 8 ya disk uhifadhi / storage ( GB 16 kwa jelly pro )
__ Betri ya M Ah 950, kutokana na udogo wa diaplay/ scren kiwango hichi ni sahihi na hakina tatizo
__ Mp2 kwa kamera ya self na mp8 kwa kamera kuu
__ Teknolojia ya Wi-Fi
__ Toleo la Bluetooth 4.0
Simu hii inaweza kuwa nzuri sana kama simu yako ya pili.
Kuweza kukusaidia kuibeba ata sehemu ambazo ungekuwa na wasi wasi wa kupoteza au kuibiwa simu yako ya gharama zaidi.
Inatengenezwa na moja ya kampuni ifahamikayo kwa jina la unihertz ya jijini shanghai
Asante sana rafiki
Maoni
Chapisha Maoni