Roho Mtakatifu Anaweza Kutumia Ukiwa Ili Kukuongoza Ktk Maisha Yako
Unachotakiwa kujua mapema ni kwamba ndani ya Roho Mtakatifu hakuna ukiwa lakini roho mtakatifu anaweza kutumia ukiwa anaoukuta mahali ambapo watu wanakaa au wanapotakiwa kukaa.
Biblia inatueleza na kutufahamisha ktk ( mwanzo 1:1 ) ya kuwa hapo mwanzo mungu aliziumba mbingu na nchi na wakati huo huo mstari unaofuata unatufahamisha ya kuwa nchi ilikuwa ukiwa tena utupu na giza ( mwanzo 1:2 )
Ukisoma mistari hii kwa haraka ni rahisi kufikiri ya kuwa mungu aliumba nchi pamoja na ukiwa na utupu taarifa tofauti.
Tunajifunza ktk somo la leo jinsi Roho Mtakatifu anavyotumia ukiwa kumwongoza mtu na kwa ajili hiyo hebu tusome ( isaya 45: 18 )
Tuone inasemaje juu ya ukiwa. Mstari huu unasema hivi " maana Bwana aliyeziumba asema hivi yeye ni mungu ndiye aliyeiumba dunia na kuifanya ndiye aliyelifanya imara hakuiumba ukiwa aliumba ili ikaliwe na watu mimi ni Bwana, wala hapana mwingine"
Ni dhahiri ya kwamba mungu hakuiumba dunia iwe ukiwa kwa hiyo hakuiumba nchi pamoja na ukiwa ila mungu aliiumba dunia ikaliwe na watu.
Hii inatupa kujua ya kuwa ukiwa na watu havitakiwi kukaa pamoja palipo na watu hapatakiwi kuwa na ukiwa na palipo na ukiwa hapatakiwi watu kukaa.
Hii ina maana ya kwamba kuna jambo ambalo halijawa wazi juu ya kile kilichotokea kati ya ( mwanzo 1:1 ) ( mwanzo 1:2 ) ikiwa kufuatana ( isaya 45: 18 )
Ukiwa haukuumbwa na mungu ukiwa wa ( mwanzo 1:2 ) ulitoka wapi ( Ezekiel 15:8 ) inatupa jibu la swali hilo mstari huu unasema hivi.
Nami ni taifa kwa sababu wamekosa asema Bwana mungu kosa lililosababisha ukiwa. ( mwanzo 1:2 ) lilifanyika lini na lilifanywa na nani Biblia iko kimya juu ya jambo hili kwa hiyo pamoja na kwamba mungu hakuumba dunia pamoja na ukiwa ( isaya 45: 18 )
Lakini baadaye ( na Biblia haisemi ni lini ) mungu aliifanya nchi kuwa ukiwa ili iwe ishara ya taarifa kwa mwanadamu ya kuwa kuna kosa lililofanyika na kwamba linatakiwa lirekebishwe kabla watu hawajaruhusiwa kuishi au kufanya kitu kwenye hilo eneo
Hii ina maana ya kwamba Roho Mtakatifu akikupa kujua kuwepo kwa hali ya ukiwa ujue anataka ufahamu huu ya kuwa kuna jambo linalohitaji matengenezo ktk ulimwengu wa roho
Ukifuatilia jambo hili kwa makini ktk Biblia utaona ya kwamba ukiwa unaweza ukawa juu ya Eneo au juu ya mtu Binafsi au juu ya kikundi cha watu
Maoni
Chapisha Maoni