Mapandaji wa farasi mweupe
Maono hayo yanaanza hivi: " Nami nikaona, na, tazama! Farasi mweupe, na yule anayeketi juu yake alikuwa na upinde, naye akapewa taji, naye akaenda akishinda na kukamiisha ushindi wake. ( ufunuo 6: 2 ) mpandaji wa farasi mweupe ni nani kitabu hicho hicho cha Bibia cha ufunuo kinamtambuisha, na kinamtaja mpanda farasi huyo wa mbingu ni kuwa "Neno a mungi. " ( Ufunuo 19:11-13 ) Neno ni jina a cheo a yesu kristo, kwa kuwa yeye ni msemaji wa mungu. ( Yohana 1, 1, 14 ) kwa kuongezea, yeye huitwa "mfalme wa wafame na Bwana wa mabwana na pia anaitwa mwaminifu na wa kweli ( ufufuo 19: 11, 16 ) kwa hakika, yesu ana mamlaka ya kutenda akiwa mfalme jasiri wa vita, naye hatumii mamlka yake vibaya au kwa ufisadi. Hata hivyo, maswali fulani yanazuka.
Ni nani anayempa yesu mamlaka ya kushinda? ( Ufunuo 6:2 ) Nabii Danieli ktk maono aliona masihi anayefananishwa na " mwana wa binadamu" akipewa " utawala na heshima na ufalme" na mzee wa siku, yaani, yehova mungu. ( Daniel 7:13, 14 ) Hivyo, ni mungu mweza yote anayempa yesu nguvu na haki ya kutawala na kutekeleza hukumu. Farasi mweupe anawakilisha vita vya haki vinavyotekelezwa na mwana wa mungu, kwa kuwa mara nyingi maandiko hutumia rangi nyeupe kuwakilisha uadiifu ( ufunuo 3:4, 7:9, 13, 14.
Wapanda farasi wa kwanza, yesu, alianza mbio baada ya kupokea taji. ( ufunuo 6:2 ) yesu aliwekwa rasmi lini kuwa mfalme mbinguni? Haikuwa baada ya kufufuliwa na kurudi mbinguni? Haikuwa baada ya kufufuliwa na kurudi mbinguni. Biblia husema kwamba alingojea kwa kipindi fulani. ( waebrania 10:12, 13 ) yesu aliwaeleza wafuasi wake kuhusu ishara ambazo zingeonyesha mwisho wa kipindi hicho, na kuanza kwa utawala wake huko mbinguni.
Alisema kwamba, baada ya kuanza kutawala, hali duniani zingebadilika na kuwa mbaya sana.
Kungekuwa na vita, upungufu wa chakula, na magonjwa ( mathayo 24:3, 7, Luka 21:10, 11 )
Muda mfupi baada ya vita vya Kwanza vya Dunia ktk mwaka wa 1914? Ili kuwa wazi kwamba wanadamu walikuwa wameingia kipindi hicho kigumu ambacho Biblia hukiita"siku za mwisho" 2Timotheo 3:1, 5.
Hata hivyo, kwa nini hali duniani zimekuwa mbaya tangu yesu alipowekwa kuwa mfalme mwaka wa 1914?
Kwa SABABU , wakati huo yesu alianza kutawala mbinguni, na si duniani. Kisha vita vikatokea mbinguni, mfalme aliyewekwa rasmi, yesu, anayeitwa mikaeli, akamtupa shetani na malaika zake duniani ( ufunuo 12:7-9, 12) Tangu wakati huo shetani amekuwa na hasira kali, kwa kuwa anajua kwamba ana wakati mfupi. Bila shaka, hivi karibuni mungu atatimia mapenzi yake kwa kumwondoa shetani hapa duniani. ( mathayo 6:10) sasa, acheni tuchunguze jinsi wapanda farasi wengine watatu wanavyothibitisha kwamba tunaishi ktk siku za mwisho zilizo ngumu. Hata hivyo, tofauti na mpanda farasi wa kwanza ambaye anawakilisha mtu hususa, wapanda farasi watatu wanaofuata wanawakilisha hali zinazowakumba wanadamu duniani kote.
Kuwa nami juma lijalo hapa hapa msikivu blog
Maoni
Chapisha Maoni