Juma lililopita, tulijifunza mpanda farasi mweupe. Tukaona mwanzo wa maono pili tukajifunza mpanda farasi huyo ni nani? Tukajua Ni nani anayempa yesu mamlaka ya kushinda.
Sasa Leo tunaendelea na somo hili tutagusia mpanda farasi mwingine rangi ya moto.
Karibu tujifunze kwa pamoja sehemu ya pili
" Na mwingine akatokea, farasi mwenye rangi ya moto, na yeye anayeketi juu yake akapewa ruhusa ya kuondoa amani duniani ili wauane, naye akapewa upanga mkubwa." Ufunuo 6:4
Mpanda farasi huyo anawakilisha vita. Ona kwamba anaondoa amani, si ktk mataifa machache tu bali duniani kote.
Mwaka wa 1914, kwa mara ya kwanza ktk historia, kulitokea vita ambavyo vilienea duniani kote. Kisha, vikafuatiwa na vita vya pili vya dunia ambavyo vilisababish mdhra makubwa zaidi.
Takwimu fulani hukadiria kwamba zaidi ya watu milioni 100 wamekufa kutokana na vita na mapigano tangu mwaka 1914 kwa kuongezea, maelfu ya watu waliteseka kutokana na majeraha mabaya ya vita.
Vita vinaweza kusababisha madhara kwa kiwango gani leo?
Kwa mara ya kwanza ktk historia, inaonekana kwamba mwanadamu ana uwezo wa kuangamiza jamii yote ya wanadamu. Hata mashirika ya kufanya amani, kama vile umoja wa mataifa, yameshindwa kukomesha vita bina to sa banishes na mpanda farasi wa rangi ya moto.
" Asante sana rafiki tukutane hapa hapa msikivu blog juma lijalo "
Maoni
Chapisha Maoni