Malaika ni nani ?
Biblia inasema nini? Kabala ya mungu kuumba ulimwengu na wanadamu, tayari alikuwa ameumba viumbe wenye akili sana kuliko wanadamu.
Wana nguvu nyingi kuliko wanadamu, nao wanaishi mbinguni pamoja na mungu, mahali ambapo wanadamu hawawezi kuingia au kupaona. ( ayubu 38: 4,7 ) ktk Biblia, viumbe hao wenye uwezo mkubwa wanaitwa " roho " au " malaika " zaburi 104:4
( Biblia husema kwamba baadhi ya viumbe wa roho waliasi mamlaka ya mungu, na malaika hao wabaya wanitwa " roho waovu " Luka 10:17,20 )
Kuna malaika wangapi? Wengi sana.
Malaika wanaokizunguka kiti cha enzi cha mungu ni " makumi ya maelfu ya makumi ya maelfu na maelfu ya maelfu " ( Ufunuo 5:11 ) Ikiwa usemi huo si wa mfano, basi kuna mamia ya mamilioni ya malaika
" Nami nikaona .... Malaika engi kuzunguka kile kiti cha ufalme..... Na hesabu yao ilikuwa makumi ya maelfu ya makumk ya maelfu na maelfu ya maelfu. " - ufunuo 5:11
Malaika ni jeshi la mungu wanaoishi na mungu mbinguni wakifanya kazi za mungu pamoja na wana wa mungu yani binadamu hapa duniani.
Ukweli sio rahisi kumuona malaika wa mungu kwa macho yetu haya ya nyama bali tunaishi nao kwa imani, kwa kuamini tu, maana maandiko yanasema hivi " Tunalindwa na nguvu za mungu kwa njia ya imani "
Wanatenda kazi zao na kuwalinda watu wanotembea na neno la mungu je unataka kulindwa na malaika?
Basi tembea na neno la mungu kwa maana malaika hawa wanasikia neno la mungu wala sio neno lako wewe mwanadamu.
Wako haina mbili za malaika
1: malaika w nuru
2: malaika wa giza
Malaika wa giza
Malaika wa giza ndio mashetani ni wahasi, walihasi neno pamoja na mamlaka za ufalme
Malaika hawa ni wakolofi ndio wanaoleta magonjwa kwenye familia, kifo, vita, njaa nk
Wanachuki dhidi ya mungu na ufalme wake na wanawake pia.
Hawapendi kuona maendeleo ya wana hawapendi kabisa.
Makao yao makubwa ni kuzimi.
Pia malaika hawa wanapatikana kwa waganga wa kienyeji kwa wachawi, wasoma nyota, madabii wa uwongo huku ndiko wanapo kaa kwa watumishi wao.
Kwa leo tunaishia hapa asante sana rafiki usikose makala yeyote hapa hapa msikivublog karibu tena juma lijalo
Maoni
Chapisha Maoni