Watu wengine wanapika maandazi ya kawaida, sasa leo angali haya na ujaribu kutengeneza utaona tofauti yake iko wapi.
Sasa endelea ili upate matokeo nakutakia uandaaji mwema.
MAHITAJI
Unga wa ngano kilo moja
Maziwa nusu lita
Samli au butter nusu kikombe
Hiliki iliyosagwa kijiko kimoja mfuto
Vanilla kijiko kimoja cha chai ( vanilla ya maji )
Maji kikombe moja na nusu
Mafuta nusu lita
Mayai mawili
Hamira ya chenga kijiko kimoja cha chakula
Jinsi ya kukanda
Kwanza chuka maji kidogo pasha moto yawe vuguvugu yenye umto mdogo kama kikombe kimoja kisha weka kwenye bakuli ndogo halafu weka ile hamira na unga ngano vijiko viwili kisha koroga vizuri na ufunike uache iumuke.
Chukua ile samli au butter ipashe moto mpaka iwe moto kabisa
Sasa chukua bakuli pana weka unga halafu mwagia yale mafuta uliyochemsha na ukoroge kwa kutumia kijiko ili usiungue mikono baada ya hapo sasa utauvuruga kwa mikono ili unga na mafuta ya changanyike vinzuri halafu utaweka tena mayai utayavunjia kwenye mchanganyiko wa unga na utavurugia kwenye unga.
Baada ya hapo utachukua hamira ambayo imeumuka na utaweka na vanilla na maziwa utaanza kukanda mpaka uhakikishe kwamba huu unga umekandika na utautengeneza duara zuri utautengeneza duara zuri utaufunika ili uumuke
Jinsi ya kuchoma
Unga ukishakuwa tayari na umeumuka utagawanisha madonge mawili au matatu na utaanza kusukuma na kukatakata kwa mpangilio mzuri na kisha utaweka kwenya sahani kubwa na utaweka pembeni.
Sasa chukua karai lako la maandazi weka mafuta na bandika mwenye moto yakisha pata moto anza kuchoma mandazi yote mpaka umalize na yasiwe brown sana ila yawe na rangi ya kuvutia. Weka kwenye chombk chako nadhifu iko tayari kuliwa na chai yako nzito ya maziwa itakayofungua mishipa ya fahamu.
Maoni
Chapisha Maoni