Nacho kiona mbele ya mziki huu wa Tanzania ni mziki kushuka kwa spidi ya ajabu sana. Napenda kusema kuwa mziki na kiki haviwezi kukaa chungu kimoja kwa maana kiki ni maisha asilia ya mtu na mziki ni ulemwengu wa hisia zinazo ishi kabisa.
Kutumia maisha yako ili kukuza mziki wako ni kupoteza muda wako pamoja na kupata madhala makubwa katika maisha yako.
Madhara utakayo yapata ni haya
1: utapoteza utu wako
2: utaishi maisha ya mashaka
3: kukosa ubunifu wa kazi zako
4: familia watakosa amani na imani na wewe
Je wewe ni mwanamuziki unaye penda sana kutumia kiki kwa ajiri ya kazi zako ?
Umepoteza nini mpaka sasa baada ya kutumia kiki ? haya ni maswali ya kujiuliza kabla ya kuamua kutubu.
Kwanini kupoteza utu wako sababu ya kuwaweka mashabiki wako moyo juu juu,
Una huwakika kweli mashabiki wako wanakupenda ? Kama kweli wanakupenda wajaribu kwa kupeleka Albamu zako soko tuone kama watanunu
Ukweli mashabiki hawana upendo wadhati, anayekupenda ni mungu na familia yako basi
Kitu kingine ni wewe kufahamu kuwa hizo sio tamaduni za mtu mweusi, pili tuna dini zetu tatu tumezungukwa na jamaa na marafiki wa familia zetu
Namaliza kwa kusema kuwa, mwaka huu ukikatika kaa mezani ujue umetengeneza shilingi ngapi
Je jamii wanakuzungumziaje na pia viongozi wako wa kidini wako tayari kukushirikisha na wamekushirikisha mara ngapi ndani ya mwaka huu
Asante sana rafiki
Maoni
Chapisha Maoni