Mojabya maswali ninayoulizwa na kulalmikiwa sana na watu wenye umri mkubwa ni uwepi wa ganzi na hisia za kuchoma na kama pini miguuni.
Ingawa dalili hizi zinaweza kutokea kokote pale mwilini ikiwemo mikononi, vidoleni, mabegani.
Kuna sababu nyingi za kujitokeza kwa hali hii ikiwamo pale unaposimama au kukaa mahali pamoja muda mrefu.
Majeraha ya shingo au pingiri za mgongo yanaweza kusababisha ganzi na kuchomachoma ktk mabega na mgongo.
Kama mtu atakuwa na majeraha ktk mgongo au kiuno anaweza pia kupata ganzi ktk maeneo ya miguuni.
Uwepo wa mgandamizo unaoleta shinikizo ktk mishipa ya fahamu inayotokea ktk uti wa mgongo mfano santuri za mgongo zinapi choropoka.
Shinikizo ktk mishipa ya fahamu baada ya kugandamizwa na mshipa ya damu uliotuna, uvimbe, kovu la tishu na uwepo wa uambukizi yote yanasababisha ganzi.
Maambukizo ya virusi vya mkanda wa jeshi, damu kuwa chache au kutofikia sehemu fulani mwili ikiwamo kujeruhiwa na theluji au mishipa ya damu kuharibika.
Kuwa na kiwango kisicho cha kawaida cha madini mbalimbali ikiwamo kalsiumu, potasiamu na sodiamu.
Ukosefu wa vitamini B na viatamini nyingine pamoja na virutubisho mbalimbali mwilini pia ni mojawapo ya ganzi mwilini .
Pia matumizi ya dawa za matibabu ikiwamo dawa za kifua kikuu ( TB ) na kufubaza makali ya VVU huambatana na hali hii.
Matibabu ya mionzi nayo yanambatana na kujitokeza kwa ganzi mwilini.
Vitu kama madini ya risasi, pombe na kemikali tiba za kutibu saratani huweza kusababisha ganzi mwilini kwani zina haribu mishipa ya fahamu.
Kuumwa na wadudu au wanyama ikiwamo nyoka, buibui, nge na aina ya mijusi wakubwa na jamii ya viumbe wa baharini pia kunaweza kuleta ganzi.
Maradhi ni kama vile kisukari, kipanda uso, ugonjwa wa kinga, kifafa nk
Asante sana juma lijalosuluhisho la ganzi hapa msikivu blog
Maoni
Chapisha Maoni