Ktk baadhi ya familia watoto wanatarajiwa wasaidie kufanya kazi za nyumbani, nao hufanya hivyo bila kulalamika.
Ktk familia nyingine, wazazi wamepuuza jambo hilo na watoto wanafurahi kwamba hawapewi kazi.
Watafiti wameona kwamba hali hiyo imeenea sana ktk nchi za magharibi, ambako watoto wanaonwa kuwa watoaji.
Mzazi anayeitwa steven alisema hivi: " leo, watoto huachwa wacjeze michezo ya video, watumie inteneti, na kutazama televisheni.
Wanatarajiwa kufanya mambo machache sana ." wewe una maoni gani ? Je, kweli kazi za nyumbani ni muhimu ili kudumisha hali nzuri ya nyumbani na vilevile ktk ukuzi wa mtoti ?
Mambo unayo hitaji kujua
Baadhi ya wazazi husita kuwapatia watoto wao kazi za nyumbani, hasa ikiwa tayari ratiba ya juma ya mtoto ina mambo mengi kama vile kazi za shuleni na utendaji wa baada ya shule. Hata hivyo, fikiria za kufanya kazi za nyumbani.
- kazi za nyumbani huchangia ukuzi wa mtoto.
- kazi za nyumbani huwaandaa watoto kuwatumikia wengine
- kazi za nyumbani huchangia umoja wa familia
MAMBO UNAYOWEZA KUFANYA
- Anza kuwa Zoeza tangu wakiwa wachanga
- wape kazi kulingana na umri wao
- tanguliza kazi za nyumbani
- kazia lengo badala ya matokeo
- kazia thawabu kuu
Maoni
Chapisha Maoni