Lugha kuu: kihispania, kibasque, kikatalani, kigalisiani na kivalencia
Idadi ya watu: 46, 439, 000. Miji mkuu Madrid
Hali ya hewa: hutofautiana, kuna majira ya kiangazi na ya baridi kali
Hispania ni inchi yenye watu wa jamii mbalimbali na mandhari tofauti tofauti. Maeneo mengi nchini humo hulimwa ngano, mizabibu, na mizeituni.
Upande wa kusini, hispania imetenganishwa na bata la afrika na sehemu ya bahari yenye upana wa kilometa 14.
Watu wengi kutia ndani wafoinike, wagiriki, na wakarthage walihamia nchi hiyo iliyo kaskazini magharibi mwa bara la ulaya.
Waroma walipoiteka inchi hiyo ktk karne ya tatu k.w.k., waliita hispania. Kisha, wakigothi na waarabu waislamu walihamia nchini humo, nao waliacha kumbukumbu za tamaduni zao.
Hivi katibuni ktk kipindi cha mwaka mmoja, zaidi ya watalii milioni 68 walitrmbelea Hispania. Wengi hutembelea Hispania ili wafurahie kuota jua, fukwe maridadi, sanaa, historia, na majengo
Jiji la toledo lina historia na utamaduni mwingi wa inchi ya hispania. Ktk mwaka 1986, jiji hilo lilichaguliwa kuwa eneo linalopaswa kuhifadhiwa Duniani na ni kivutio kikuu cha walii
JE, WAJUA ?
Nchi ya Hispania inaongiza duniani kwa uzalishaji wa mafuta ya zeituni.
Mlima Teide wenye urefu wa futi 12,198 ( 3,718 m ) na ulio kwenye visiwa vya canary, ndio mlima mrefu zaidi nchini Hispania. Unapopimwa kuanzia kwenye kina chake kilicho baharini, mlima Teide ni wa tatu kwa urefu kati ya milima mingine ya volkano duniani.
Vyakula vya Hispania
Vyakula vya Hispania huwavutia watu wengi wanaotembelea huko. Vyakula vya asili hutia ndani viumbe wengi wa baharini, vipande vyembamba vya nyama ya nguruwe, mchuzi uliotayarishwa vizuri, kachumbari na mboga zilizotiwa au kupikwa kwa mafuta ya zeituni
Wahispania ni watu wachangamfu na wenye urafiki
Asante sana
Maoni
Chapisha Maoni