Nyuki anaweza kutua salama mahali popote bila tatizo. Anawezaje kufanya hivyo?
Fikiria jambo hili: ili atue salama, nyuki anahitaji kupunguza mwendo wake kabisa kabla ya kugusa mahali anapotaka kutua. Nija moja rahisi ingekuwa kupima kasi yake na umbali wa kufika pale anapokusudia kutua, kisha punguze kasi hiyo hatua kwa hatua kulingana na umbali uliobaki.
Hata hivyo, njia hiyo ni ngumu kwa wadudu wengi, kwa sababu wana macho ambayo hayawezi kupima umbali.
Macho ya nyuki yanaona kwa njia tofauti sana na ya mwadamu anayeweza kuona na kukadiria umbali. Inaonekana nyuki hutumia njia rahisi ya kwamba kadiri anavyosogelea, kitu hicho kinazidi kuonekana kikubwa. Kadiri anavyozidi kukikaribia, kinazidi kuongezeka ukubwa kwa kasi zaidi.
Uchunguzi uliofanywa na Australian Nationl University unaonyesha kwamba nyuki hupunguza mwendo wake ili kasi ya kuongezeka ukubwa wa kitu anachotazama ibaki vilevile.
Anapilofika mahali alipikusudia kutua, mwendo wake unakuwa umepungua sana, na hivyo kumwezeaha kutumia salama.
Jarida la proceedings of the National Academy of Science liliripoti hivi: " Mbinu hii rahisi ya kutua .... Itafaa sana ikiwa itatumiwa ktk mfumo wa kuongiloza roboti zinazoruka angani."
Una maoni gani ? Je, mbinu ya nyuki ya kutua ilijitokeza yenyewe ? Au ilibuniwa ?
Maoni
Chapisha Maoni