BERI ndogo aina ya Pollia condensata, inapatikana barani Afrika. Beri hii ina mwonekano wa bluu unaong'aa sana kuliko mmea mwingine wowote.
Hata hivyo basi, ni nini hufanya iwe na mng'ao wa bluu?
Fikiria: Chembe zilizo kwenye ngozi ya beri zina kuta zenye nyuzinyuzi nyembamba sana ambazo zimepangwa kama safu ya njiti za kiberiti.
Nyuzimyuzi hizo hufanyiza matabaka, kila tabaka likiwa limepinda kidogo ukilinganisha na la chini yake, na hivyo kufanyiza umbo la springi.
Nyuzinyuzi hizo hazina rangi ya bluubkwa sababu ya jinsi zilivyopangwa. Hivyo, kinachotokeza mwonekano wenye kung'aa, unaobadilika badilika si rangi bali ni mpangilio wa nyuzinyuzi.
Chembe nyingi huonekana kuwa za bluu. Lakini zinapotazamwa kutoka pande tofauti tofauti, zinaonekana kuwa za kijani, waridi, au njano ikitegemea matabaka hayo.
Kwa kuongezea, zinapochunguzwa kwa makini, beri hizo huonekana kuwa na madoadoa kama vile rangi kwenye skrini ya kompyuta.
Kwa sababu hazina rangi, beri hizo hazipotezi mng'ao wake wa bluu hata zina podondoka.
Wewe una maoni gani ? Je, mng'ao wa bluu wa beri aina ya pollia ulijitokeza wenyewe tu? Au ulibuniwa
Maoni
Chapisha Maoni