MPAKA SASA ARGENTINA WANA POINT 25 SAWA NA PERU, lakini waperu wapo juu kutokana na tofauti ya mabao na endapo Argentina itafungwa ktk pambano hilo la kufa na kupona basi ndoto zao za kushiriki kombe la dunia mwakani zitakuwa zimekoma.
Wakati huo huo pambano la mwisho pa peru na colombia kama litamlizika kwa sare huku lile la Argentina na Ecuador likimalizika kwa sare, basi ndoto za Argentina kwenda kombe la dunia mwakani zitakuwa zimekoma.
Endapo kama peru akidungwa na Argentina wakipata sare, basi Argentina watalazimika kucheza pambano la mtoano dhidi ya mshidi kutoka Bara la oceania ambao ni New zealand.
Endapo Argentina itashindwa kufuzu kombe la Dunia mwakani litakuwa pigo kubwa kwa kizazi cha sasa cha Argentina ambacho kimesheheni mastaa wengi
Argentina haijashinda taji lolote tangu ilipotwaa kombe la copa Amerika mwaka 1993
Kwa sasa messi ana umri wa miaka 30 na haionekani kama ataweza kucheza ktk fainali za kombe la Dunia za Qatar mwaka 2022 akiwa na umri wa 36
Maoni
Chapisha Maoni