Kagonjwa ya kuambukiza yapi ya aina nyingi. Magonjwa hayo huenezwa kwa njia mbalimbali. Ili kuzuia kueneza ni muhimu kuzibgatia usafi wa mtu binafsi na wa mazingira.
Magonjwa hayo ni kama vile, kuhara, kichocho, malaria nk
Kuhara
Huuni ugonjwa unaoletwa na vijidudu vinavyosababisha uvimbe wa tumbo.
Ni ugonjwa wa kwenda haja kubwa mara nyingi kupita kiasi kwa siku moja
Dalili
. mgonjwa hujihisi msokoto wa tumbu
. Huenda haja kubwa laini sana mara nyingi kwa siku ( mara sita au zaidi )
. Ulimi huwa mkavu
. Wakati mwingine huweza kutapika.
Ugonjwa unavyoenea
Kuhara ni ugonjwa unaoenezwa kwa kunywa maji machafu. Pia ntu akila chakula kilichoguswa na inzi huweza kuharisha.
Jinsi ya kujikinga na kuhara
. Ili kujikinga na ugonjwa wa kuhara zingatia mambo yafuatayo
. kunywa maji safi na salama
. Tumia choo kwa haja kubwa na ndogo
. Funika chakula ili inzi asiguse
. Nawa mikono kwa sabuni kabla na baada ya kula
. Safisha na menya natunda kabla ya kuyala
Nimekupa bahazi ya mambo kifupi wewe mwenyewe unapaswa kuwa msafi, mazingira yako pia pamoja na mavazi yako, Asante sana rafiki juma lijalo nitakuletea magonjwa mengine ili ujue kujikinga nayo. asante sana
Maoni
Chapisha Maoni