Jina zuri, au heshima, lina thamani sana hivi kwamba ktk baadhi ya nchi linalindwa kisheria.
Hilo linaweza kutia ndani kulinda jina lisichafuliwe kupitia maandishi au kwa maneno.
Jambo hilo linatukumbusha usemi huu wa kale; " Ni afadhali kuchagua jina badala ya utajiri nwingi; kibali ni bora kuliko hata fedha ba dhahabu." ( methali 22:1 ) Tunaweza kufanya nini ili tuwe na jina zuri na kuheshimiwa na wengine ? Mapendelekezo bora zaidi yanapatikana kwenye Biblia.
Kwa mfano, fikiria yale ambayo Biblia inasema ktk ( zaburi ya 15 ) ili kujibu swali,
" Ni nani atakayekuwa mgeni ktk hema la [ Mungu ] ? "
Mtunga zaburi aliandika hivi: " yeye..... [ anayezoea ] kutenda uadilifu na kusema kweli ktk moyo wake.
Yeye hakuchongea.... Hakumfanyia mwenzake jambo lolote baya, wala hakumshutumu rafiki yake.
Machoni pake mtu yeyote nwenye kudharaulika hakika amekataliwa.... Ameapa juu ya jambo lililo baya kwake, na bado yeye habadiliki... Wala hakuchukua rushwa. " ( zaburi15: 1,5 ) Bila shaka utamheshimu mtu anayeishi kupatana na kanuni hizo, sivyo ?
Sifa nyingine inayoweza kufanya ntu aheshimiwe ni unyenyekevu.
Andiko la methali 15:33 linasema hivi: " kabla ya utukufu hutangulia unyenyekevu huona sehemu anazohitaji kufanyia maendeleo naye hujitahidi kuziboresha.
Pia yuko tayari kuomba msamaha kwa hiari anapomkosea mwingine.
( yakobo 3:2 ) Tofauti na hilo, mtu mwenye kiburi hukasirika upesi na kujitetea. Methali 16: 18 inasema hivi: " kiburi hutangulia kujikwaa."
Hata hivyo, namba gani ikiwa mtu fulani amechafua jina lako? Je, utachukua hatua haraka, labda ukiwa na ghadhabu nyingi ?
Jiulize hivi, " ikiwa nitajitahidi kutetea jina langu, je, sitakuwa nikieneza zaidi uwongo huo? Ingawa nyakati fulani inaweza kufaa ushauri huu wenye hekima: " usiende kwa haraka kufanya kesi." ( methali 25: 8,9 ) kushughulikia mambo kwa njia hii kunaweza pia kuokoa pesa nyingi ambazo ungetumia kuendeshea mashtaka.
Biblia si kitabu cha kidini tu. Ni mwongozo unaotegemeka wa maisha. Wote wanaofuata hekima yake wanasitawisha sifa zinazofanya waheshimiwe sana na kupata jina zuri.
Jinsi ya kutengeneza sabuni ya maji Malighafi: 1. Sulphonic Acid Lt 2 2. Soda Ash Kg 1 3. Sless Lt 1 4. Chumvi Kg 1 5. Pafyumu /rangi Bluu 6. Maji Lt 35 _ 40 Jinsi ya kutangeneza Anza kwa kuweka lita 10 mara tatu, yaani lita 10 tena na mwisho lita 10, angalia uzito ongeza tena lita 5 na kisha lita 2 ikiwa uzito bado ongeza lita 2 na mwisho lita 1 4. Chumvi kg 1 3. Sless Lt 1 2. Soda Ash Kg1 1. Sulphonics Acid Lt 2 Hapo sijaweka rangi wala pafyumu kwa sababu ukiweka pafyumu lita 35 bila kufunika itaisha baada ya muda mfupi. Ni vema rangi na pafyumu uweke pembeni. Mfano: Chukua ndoo ya lita 10, weka rangi robo kijiko cha chai na pafyumu vijiko vya chakula viwili na koroga vizuri. Ni vema utumie pafyumu aina ya lemon. Sababu za kutoweka rangi sabuni yote: Wapo wateja hawapendi rangi na harufu kwa hiyo utawapa kila mtu kama atakavyo na kujaza kwenye chupa zako zenye mifuniko saa hiyo hiyo ukiachia muda inatoka harufu. Asante sana rafiki.
Maoni
Chapisha Maoni