Vijidudu, yaani bacteria, ni vidogo mno navyo havionekani kwa macho matupu, ila kwa darubini tu, lakini vina uhai, hujilisha na kujiongeza kwa upesi sana. vijidudu hivi vyapatikana po pote ktk vumbi, takataka, udongo, mimea na chakula.
Vimo vile vile ktk ngozi yetu na ya wanyama, hata ktk ngozi ile nyororo.
Vimo kinywani, kooni mpaka tumboni kuyeyusha chakula navyo hutoka pamoja na kinyesi.
Lakini havipatikani ktk viungo vingine vilivyofunikwa kama vile musuli, moyo, maini, mishipa ya damu na kadhalika.
Kabisa havipatikani ktk kibofu au ktk mji wa mimba wala ndani ya mimba.
Vijidudu vyo vyote vile viingiapo ktk viungo hivyo huviharibu kabisa.
Basi tuangalie sana tusiingize vijidudu hivyo ktk viungo kutoka ktk ngozi au ktk kinyesi, sababu ingawa vitaingia vijidudu huitwa kiungo safi kabisa ( sterile )
Ktk vijidudu vile vyenye maana yaani viyeyushavyo chakula tumboni hivi hudhuru sana vikiingia ktk viungo vinginevyo.
Vile vile tukiingiza mrija wa kutolea mkojo ktk kibofu na hivyo hudhuru sana; yaani baada ya siku chache hutokea ugonjwa wa kibofu uitwao kwa kiganga Cystist.
Vivyo hivyo tumpimapo mzazi wakati wa kuzaa au wakati wa kutoa kondo kwa mikono au vyombo visivyo safi kabisa basi twamwambukiza vijidudu.
Kuambukiza hakuonekani Mara kwa kuwa vijidudu hutuia siku au muda fulani mpaka vimejizidisha na kuwa vingi vya kutosha na kutoa maradhi.
Muda huo huitwa muda wa kujizidisha ( the incubation period ) lakini muda huo watofautika kwa kila maradhi, kwa kawaida huchukua siku chache tu.
Vijidudu viletavyo maradhi vyapangika hasa ktk aina nne:
1: Cocci vyenye sura ya vinukta.
2: Bacilli vyenye sura ya vistari
3: Spiroketi vyenye sura ya vijinywele vilivyopindana.
4: Vires ni vijidudu vya maumbile ya pekee vidogo sana kuliko bacilli na havionekani kwa darubini ya kawaida.
Aina yo yote ya vijidudu akiambukizwa nayo mama mzazi huugua sana.
Habari hizi zote hazijuliwi na wakunga wenyeji wasiojua ku soma.
Wao hueleza ajali mbaya kuwa ni matokeo ya kulogwa, ama adhabu ya kuvunja mwiko na kdhlika.
Hivyo huwa hawafaulu ktk uzazi wenye taabu na shida hasa waingizapo mikono michafu ukeni au ktk mji wa uzazi.
Ni dhahiri wazazi huuawa na wakunga wenyeji ingawa huwa na nia njema ya kusaidia.
Njia za kuua vijidudu
Yajulikana kuwa hakuna vujidudu viwezavyo kuishi muda mrefu ndani ya maji ya kuchemka au mvuke wake.
Kwa hiyo twafahamu kuwa vyombo vyote vitumikavyo ktk ukunga visivyodhurika na maji ya moto lazima vichemshwe ktk maji u mvuke wake.
1. Vyombo vya madini kama vile koleo, vibano na sahani na kadhalika, hivi vyote vitiwe ndani ya maji ya kuchemka kwa muda wa dakika 20. Kuhifadhi makali ya visu yafaa kuvifunika na pamba tena vitiwe ndani ya alcohol.
2. Vyombo vyote vya mpira vichemshwe vile vile lakini kwa muda wa dakika 5 tu. Baadaye vifunikwe na kitambaa safi kabisa, au tunaweza kuvitia ktk boz la chuma lililifungwa kabisa pamoja na tunaweza kuvitia ktk box la chuma lililofungwa kabisa pamoja na vodonge vya Formalin kwa muda wa saa 24.
Vyombo vya namna ya bilauri kama vile bomba la sindano, kitilio vichemshwe vile vile muda wa dakika 20.
Lakini tuangalie kuvitia ndani ya maji kabla hayajachemka na vifunikwe na kitambaa
3. Nguo na vitambaa vya kufungia ( dressings ) lazima vichemshwe ktk sufuria ipitishayo mvuke kwa nguvu ( sterilizer ) humo muda wake ni mfupi kama dakika 20 tu.
Kama hakuna sterilizer unaweza kuvichemsha vitambaa ktk sufuria na baadaye kuvinyosha na pasi.
Hii siyo safi kabisa ( sterile ) lakini ni safi.
Vyombo vyote viharibiwavyo na maji ya kuchemka, hivi hufanywa safi kabisa vikitiwa ndani ya dawa zinazoua vijidudu ziitwazo Dawa hizo ni lotions
a. Lysol, sehemu moja kwa mia ( 1% )
b. Dettol 1%
c. Cetavolon, sehemu moja kwa mia ( 1% )
Namna ya kunawa mikono na ngozi viwe safi kabisa ( sterile )
1. Mikono : yatumika dakika kumi. Pete, bangili zinavuliwe, kucha zikatwe na kusafishwa sana.
a: Tunawe mikono kwa maji na sabuni muda wa dakika saba na pasipo kufuta tuitie
b: Ndani ya lotion ya Dettol 1/2% au ndani ya Lysol 1/2% au Cetavlon 1/2% Kwa muda wa dakika tatu. Kila tukichafuka, mfano, kwa kushika kitu au kiungo kisicho safi kabisa, yatulazimu tuioshe mikono yetu tena ndani ya lotion muda wa dakika chache.
2. Ngozi ya mzazi: Isafishwe kwa kitambaa laini ( gauze ) kilichochovywa ktk lotion yo yote, tupanguse mbele ( vulva ) mara tatu toka juu kwenda chini na kila mara tukitupe kitambaa anapasuiwa ( Operation ) ngozi ya juu ipakwe Tr of lodine sehemu 2,5 kwa mia ( 2,5% ) au mercurochron 1% au disinfectants nyinginezo
Maoni
Chapisha Maoni