Kila wakati tunapumua. Je ni lazima tupumue ? Hatuwezi tukakaa bila kupumua ?
Tendo la 1: Kugundya ikiwa Tunaeza Kukaa Bila Kupumua
Jaribu kutulia bila kuvuta hewa ndani. Umeweza kukaa bila kupumua kwa muda mrefu?
Mtu akizuiwa kupumua anakufa.
Hii ni kwa sababu mwili wake utakosa hewa.
Je, hewa ina umuhimu gani ktk mwili?
Chakula hutupatia nishati. Nishati hiyo hutuwezesha kufanya kazi.
Vile vile nishati hiyo huuwezesha mwili kufanya kazi ndani yake ambayo ni ya lazima kwa uhai.
Ili chakula kitupatie nishati ni lazima kibadilishwe.
Mabadiliko hayo hayawezi kutokea ikiwa mwili utakosa hewa.
Umuhimu wa maji
Mwili wa mnyama siyo mkavu kama vile jiwe.
Mwili una majimaji. Mifupa huonekana mikavu.
Lakini kwa kweli ina kiasi fulani cha maji.
Tukisikia kiu tunakunywa maji.
Kiu ni ishara ya jambo gani?
Tukisikia kiu maana yake maji yamepungua mwilini.
Hivyo, kila wakati mwili unahitaji kuwa na maji kiasi fulani.
Kwa nini mwili unahitaji maji ?
Mwili ni lazima ufanye kazi zake za ndani ambazo ni za muhimu kwa uhai.
Kazi hizo haziwezi kutendeka bila kuwepo maji. Hivyo bila maji hakutakuwa na uhai.
Asante sana kwa uwepo wako rafiki yangu
Maoni
Chapisha Maoni