Unamfahamu mtafiti mwanamke aliyewezesha nchi kupata mbegu bora za mpunga ili kukabiliana na uharibifu wa udongo?
Kituo cha utafiti wa kilimo cha chollima kilichoko, Dakawa, Morogoro kimeleta mafanikio kupitia utafiti uliofanywa na mkuu wa kituo hicho, Dk sophia Kashenge Kilenga ambaye anaongoza jopo la watafiti wa mbegu bora za mpunga.
Mtaalamu huyo aliyefanikisha kituo hicho aliyefanikisha kituo hicho kuzalisha mbegu bora zinazoweza kukabiliana na uharibifu wa udongo ktk mashamba ya umwagiliaji ya mpunga yanayokabiliwa na ongezeko la chumvi.
Mbegu za mpunga tatu ambazo mtafiti huyo amezalisha ni SATO1, SATO6 na SATO9 ambazo ni bora zaidi kukabiliani na ongezeko la chumvi ktk mashamba ya umwagiliaji mpunga.
" Mbegu moja kati ya hizo tatu, SATO1 ilidhinishwa na kamati maalumu ya mbegu iliyoko wizarani machi 18 2016"
Anasema utafiti kuwa:
" Kila mbegu ina uwezo wake wa kukua kulingana na aina ya udongo "
Anaendelea kueleza kuwa ili kuboresha utafiti huo, mwaka 2013 alianzisha mradi mwingine wa utafiti chini ya mpango wa shirika la msaada la maendeleo la kimataifa marekani
( Usaid ) iAGRI Kwa ajili ya kutafiti njia bora ya kubadili mfumo wa ardhi ktk nashamba ya umwagiliaji mpunga ya ndugu ya wilayani same, Mkoa wa kilimanjaro.
Ktk maboresho hayo ya utafiti, alisema watafiti walibaini matumizi ya madini ya Gypsum, mboji na taka zitokanazo na mabaki ya mbo zikiwekwa ardhi isiyorutubishwa.
" Matokeo haya ya utafiti wa muda mrefu ni muhimu sana kwa kuwa ongezeko la chumvi ni chachu inayoua udongo taratibu.
Kupatikana kwa tiba hii kutasaidia sana kuongeza mapato ya wakulima wa mpunga kwani chumvi imekuwa ikisababisha kupunguza kwa mapato, "
Anasema.
Matokeo ya utafiti huu pia yatasaidia wakulima wadogo wengi wa mpunga ambao wanakabiliana na umaskini.
Matokeo haya ya utafiti ni ufumbuzi wa kuongeza mapato ktk uchumi wa familia na taifa kwa ujumla kwani usalama wa chakula pia utaimarika
Maoni
Chapisha Maoni