"Kujiamini kwangu kunakuja tu nikiwa na kiatu kizuri na nikiwa na nywele za kupendeza.
Nikiwa na vitu hivyo huwa sina haja hata ya kujipodoa. Nywele zangu ndiyo utambulisho wangu. Kwa kuangalia tu nywele zangu utaweza kujua mimi ni mtu wa aina gani"
Maneno haya utayapata kwenye ukurasa wa mbele kabisa w blog yake ya http:// www.styleismythinglux.com Blog dada ya styleismy thing ambayo ni kazi ya mikono yake staa huyu.
Soraya De Carvalho ni mhariri wa blog za styleismything.net, tofauti na mabloga wengine, soraya alipata wazo la kuanzisha blog baada ya kujiuliza tu ni wapi tpt nguo zinazoendana na umbo lake?
Kujiuliza kwake swali hili kulimpa nguvu ya kwenda mbele zaidi.
Na kuamua kushiriki pamoja na wapenzi wa fasheni ktk kutoa mawazo na kuyafanyia kazi .
Soraya ni mwafrika mwenye asili ya Angola anayeishi nchini uingereza.
Mbali na kazi yake ya uandishi ktk mambo ya fasheni pia ni mjasiriamali anayejishughulisha na uuzaji wa bidhaa za nguo na nywele.
Blog
Style is my Thing
Instagram: @styleismything
Ukurasa wake wa instagram una wafuasi: 125,000
Inaendeshwa kutoka uingereza
Hapa ni fasheni kwa kwenda mbele.
Mitindo yote ya nywele na pia viatu pamoja na mavazi na mwenyewe soraya.
Ni blog mhsusi kwa wanawake wenye maumbo ya kiafrika.
Si hivyo tu hata wale wenye rangi adimu ya ngozi hapo ndipo mahala pake.
Utapata mitindo mipya ya viatu na mavazi mengine.
S I hivyo tu pia utaweza kununua moja kwa moja kupitia mtandao huu.
Uzuri wa blog hii ipo ktk mikono salama ya mtaalamu mahiri wa mitindo, hivyo itakuwa ni rahisi kwako kuangalia na hata kuingia na kuchanganya kwenye mavazi yako na mwisho wa siku ukaishia kutoka bomba.
Huna haja ya kupoteza muda, ingia kwenye blog hii na peruzi kuona kama kuna mavazi ama mtindo unaoupendelea.
Maoni
Chapisha Maoni