Madhabahu ni nini Ni mahali pa juu yanayounganisha na kupatanisha ulimwengu wa roho na ulimwengu wa damu na nyama yani ulimwengu wa mwili
Kwa nini madhabahu; madhabahu ni mlango wa kufungua mambo yasio honekana kwa macho ya nyama, ambao mlango huo unafunguliwa kwa kuangusha kafala, sadaka juu ya madhabahu.
Ni nani aliye buni jambo hili la madhabahu
Biblia aisemi ni mwanadamu gani aliyebuni jambo hili bali Biblia imetaja na kuonyesha familia ya kwanza kutumia madhabahu.
Familia ya kwanza kutumia madhabahu ni familia ya Adamu na Hawa.
Hii ndio familia ya kwanza kutumia madhabahubya bwana.
Tunafahamu kwenye ( mwanzo 4:1,4 )
Tunaona watoto wa Adamu wakisogeza sadaka kwa Bwana Neno linasema hivi " Adamu akamjua hawa mkewe naye akapata mimba akamza kaini akasema Nimepata mtoto mwanaume kwa Bwana Akaongeza akamzaa ndugu yake Habili alikuwa mchunga kondoo na kaini alikuwa mkulima ardhi ikawa hatimaye kaini akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona za wanyama. Bwana akamtakabali Habili na sadaka yake"
Sasa basi sipo hapa kufahamu yaliyotokea kwa wanandugu hawa na sadaka zao.
Bali nipo hapa ili tufahamu watu wa kwanza kutumia madhabahu ya Bwana na Tumefahamu kuwa familia ya Adamu ndio watu wa kwanza kutumia madhabahu ya Bwana, japo ktk Biblia hatuoni mahali Bwana akisema na Adamu hivi " ni jengee madhabahu yangu"
Ila tumefahamu kwa sadaka za watoto wake kwa maana uwezi kufanya jambo kama hauna maelekezo.
Bwana ndiye mwanzo wa jambo hili ( ufunuo wa yohana 8:3 ) ianasema hivi Na malaika mwingine akaja akasimama mbele ya madhabahu, mwenye chetezo cha dhahabu, akapewa uvumba mwingi, ili autie pamoja na maombi ya watakatifu wote juu ya madhabahu ya dhahabu, iliyo mbele ya kiti cha enzi.
Hata mbinguni yapo madhabahu tena ya dhahabu.
Shughuli ye yote ya kiroho lazima yaitimiswe kwenye madhabahu.
Madhabahu yetu sisi wa duniani ni mfano wa madhabahu ya mbingu.
Sikia ndugu;
Nyuma ya Mafaniko yako yapo madhabahu
Ushindi wako jua kabisa nyuma yuko mungu.
Kwa hiyo mungu anayo madhabahu fahamu kuwa hata shetani roho muongo na mchinjaji tangu mwanzo pia na yeye anatumia madhabahu
Raia wa Ulimwengu wa roho ni lazima kutumia madhabahu ili uweze kumiliki vyitu vya mwilini.
Kwa nini kumiliki
Tutajifunza jambo hili wakati ujao kwa leo tunaishia hapa
Maombi ya kuomba
Kwa damu ya mwana kondoo na vunja madhabahu za mashetani kwa jina la yesu kristo.
Madhabahu ye yote niliowaikuto sadaka nazivunja kwa damu ya yesu kristo kwa damu ya mwana kondooo, kwa damu ya mwana kondooo amen
Sasa rafiki endelea kuomba maombi haya kila siku bila kukata tamaa kwa maana hadui wetu shetani hacho rafiki na wewe usichoki si mama kwa imani kuomba maombi haya amen.
Maoni
Chapisha Maoni