Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Kanuni kum

Uhalisi wa maisha

Maisha halisi ya mwanamke anayetarajia kuwa mke/mke tayari hii ni kumaanisha kuwa wanawake mashujaa tunapaswa kuishi maishi ambayo yanatutambulisha kama mfano wa kuigwa ili tunapozungumza na kufundisha mabadiliko tuwe tunazungumza uhalisia wa maisha yetu ambao unajengwa na haya yafuatayo

Uvumilivu

Kuwa mvumilivu ktk maisha yake ya kila siku hasa ukizingatia kuwa tunakutana na mambo mbalimbali yasiyo tuvutia ktk mahusiano yetu mengine ni magumu na yanayokwenda kinyume kabisa na matakwa yetu au mazoea yetu ya binafsi.
Ifahamike kwamba wewe kama mwanamke shujaa inapotokea umekutana na mambo kama haya hupaswi kuonyesha hasira zako wazi wazi.
Kama vile chuki, kulaumu, ugomvi, vurugu, malalamiko au aina yoyote ya uharibifu kutokea kwako au ndani mwako.
Hivyo mwanamke shujaa huwa ni heri kila anapokuwa kwani hutunza amani ya eneo alipo.

Upendo wa dhati

Maisha ya upendo wa halisi na sio wa kinafki kwa jamii inayomzunguka.
Tabia ya upendo wa halisi ina thamani kubwa san kuliko mali nyingi, pesa, elimu ya juu n.k
Wewe unaweza kabisa kuwa na elimu ya juu sana pesa nyingi sana lakini pasipo upendo wa halisi ni sawa na kusema kopo zuri kwa nje na ndani hamna kitu nguzo kuu ya maisha ya mwanamke shujaa ni upendo wa dhati na uhalisia

Utii kwa Jamii

Maisha halisi ya utii ktk jamii inayokuzunguka ili kuweza kuyafanyia kazi yale yote uliyojifunza na pia kuyatenda kwa ufasaha pasipo kupita kona yoyote.
Utii kwa jamii ni ufunguo mmoja wapo utakaokusaidia kufanikisha mambo yako na malengo yako kama mwanamke shujaa

Uaminifu ktk jamii

Kuishi maisha ya uaminifu wa kweli na uhalisia ktk jamii inayomzunguka.
Uaminifu wa kweli huonekana nyakati zote na siyo tu wakati mtu anapokuwa mbele za watu wanaomjua bali hata wale wasiomjua na hata anapokuwa mahali peke yake aweze kutu mwanamke shujaa hujitahidi sana kutunza uaminifu wake ktk sekta zote

Unyenyekevu wa kweli

Kuishi maisha halisi kabisa ya unyenyekevu kwa jamii inayomzunguka, unyenyekevu ni kinyume kabisa na kiburi majivuno, kijigamba, na hata kujitanguliza mbele kwa kila jambo.
Mwanamke shujaa huwa ni mnyenyekevu wakati wote na hana makuu daima

Uwajibikaji wa dhati

Maisha halisi ya uwajibikaji akiangali majukumu yake yote yanayomkabili na kuhakikisha anafanya moyo bila kuwa na tabia ya kusaidiwa majukumu yake mwanamke shujaa ni mfano wa kuigwa kutokana na uwajibikaji wake.

Ushirikiano wa dhati

Ushirikiano ktk jamii inayomzunguka. Sisi wanawake mashujaa yatupasa kujua dhahiri kuwa kazi ya kubadili tabia na kufanya wenyine wabadilike kwa lengo la kupata familia bora ni lazima kuwa na ushirikiano wa kweli ambao utajenga tabia ya kuaminiana na kunia mamoja ktk harakati hizi za kuandaa, kujenga familia bora

Utaratibu wa kazi / mpangilio

Ktk utaratibu wa maisha yake pamoja na mpangilio mzuri wa mambo yanayomzunguka hii itakusaidia kuwa na muda mzuri wa kufanya shughuli zako na pia kutekeleza majukumu yako ya kila siku kama mwanamke shujaa.
Hakuna njia yoyote ya kukuwezesha kukua na kuendelea ktk maisha yako bila kuwa na utaratibu na mpangilio wa mambo yako.

Kufanya tathimini

Kuweza kufanya tathimini ya yale yote anayoyafanya ktk maisha yake ya kila siku pengine ni mfanya biashara, mfanya kazi, mkulima n.k
Kama mwanamke shujaa yakupasa kutathimini shughuli zako kama zina leta faida / hasara kwa familia na jamii yako inayokuzunguka.
Ukiona faida ni kubwa unaendelea na hiyo shughuli lakini kama hasara ni kubwa unajiweka ktk nafasi ya kubadilisha aina ya shughuli mara moja bila kupoteza wakati.

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Jinsi ya kutengeneza sabuni ya maji

Jinsi ya kutengeneza sabuni ya maji Malighafi: 1. Sulphonic Acid Lt 2 2. Soda Ash Kg 1 3. Sless Lt 1 4. Chumvi Kg 1 5. Pafyumu /rangi Bluu 6. Maji Lt 35 _ 40 Jinsi ya kutangeneza Anza kwa kuweka lita 10 mara tatu, yaani lita 10 tena na mwisho lita 10, angalia uzito ongeza tena lita 5 na kisha lita 2 ikiwa uzito bado ongeza lita 2 na mwisho lita 1 4. Chumvi kg 1 3. Sless Lt 1 2. Soda Ash Kg1 1. Sulphonics Acid Lt 2 Hapo sijaweka rangi wala pafyumu kwa sababu ukiweka pafyumu lita 35 bila kufunika itaisha baada ya muda mfupi. Ni vema rangi na pafyumu uweke pembeni. Mfano: Chukua ndoo ya lita 10, weka rangi robo kijiko cha chai na pafyumu vijiko vya chakula viwili na koroga vizuri. Ni vema utumie pafyumu aina ya lemon. Sababu za kutoweka rangi sabuni yote: Wapo wateja hawapendi rangi na harufu kwa hiyo utawapa kila mtu kama atakavyo na kujaza kwenye chupa zako zenye mifuniko saa hiyo hiyo ukiachia muda inatoka harufu. Asante sana rafiki.

Fahamu jinsi ya kutengeneza sabuni ya vyoo

Sabuni ya kusafisha vyoo Malighafi. 1. Sulphonics Acid Lita 1 2. Soda Ash nusu 1/2 kilo 3. Sless 4. Chumvi 1/2 kilo 5. Maji lita 17 1/2 _ 20 6. Rangi kijani 7. Pafyumu 8. Formalin Jinsi ya kutengeneza Weka maji lita 5 kisha anza kukoroga, ongeza lita 5 kisha lita 5 tena na mwisho lita 2 4. Chumvi 1/2 kg 3. Sless nusu lita 2. Soda ash nusu kilo 1. Sulphonics Acid lita 1 Hapo sijaweka rangi wala pafyumu ni vinzuri kuweka kwenye ndoo lita 10 ya sabuni utaweka rangi kijiko 1 cha chai, rangi ya kijani pafyumu aina ya ' Rose two one ' au pino vijiko 5 vya chakula na Formalin vijiko 3 vya chakula. Formalin kwa ajili ya kuua wadudu ( bacteria ) ni vinzuri sana kuwemo kwenye sabuni ya chooni kwani ina kazi nyingi zaidi ya hiyo iliyotajwa Asante sana rafiki sasa chukua hatua ya kufanya hakika utafanikiwa sana

Somo: Roho mtakatifu Na mwl Christopher Mwakasege

Kushirikiana Na Roho Mtakatifu Anapotumia Moto kukuongoza ili utembee kwenye mapenzi ya mungu Biblia inafundisha ya kuwa wana wa mungu huwa wanaishi na wanatakiwa waishi kwa kuongozwa na roho mtakatifu ( warumi 8 : 14, 16, 17 ) Njia moja wapo anayotumia roho Mtakatifu kumwongoza mwana wa mungu, ni kwa kutumia moto wa mungu anaokuja nao ndani ya mtu anapoingia kukaa kwake Biblia inasema juu ya yesu ya kuwa yeye atawabatiza kwa roho mtakatifu na kwa moto ( luka 3 : 16 ) na siku ya pentekoste, wakati wanafunzi wa kwanza wa yesu, walipokuwa wamekutanika pamoja kukuwatokea ndimi zilizogawanyika, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao wote wakajazwa roho mtakatifu ( matendo 2 : 3,4 ) Unaposoma na kutafakari jambo lililotokea siku hiyo ya pentekoste, utajua kuwa kuna uhusiano kati ya ndimi za moto juu ya kila mmoja wao na kule kujazwa roho mtakatifu kwa kila mmoja wao ni dhahiri ya kuwa roho mtakatifu anaingia ndani ya kila mwana wa mungu akiwa pia na moto wa mungu pamoja nao kazi m...