Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Jicho ovu Na Askofu josephat Gwajima

Mungu ni roho lakini ana macho kwa hakika tunajua mungu ana macho, tunaona ana macho na macho ya mungu yakikutazama unapata mafanikio, ulinzi na uponyaji

Shetani pia ana macho, ambayo macho yakikutazama unapatabmatatizo, balaa na mikosi. Maana macho ya shetani ni macho ya uovu, kuna watu wana matatizo kwa sababu jicho la uovu ( zakaria 3:9 ) ( Amos 9:8 ) ( ufunuo wa yohana 5:6 ) ( kumbukumbu la torati 15:9 )

Jicho ovu maana yake jicho la ubaya
( Torati 28:54 ) ( Torati 28:56 ) ( mathayo 20: 5 )

Macho yako ya mwili ni diriaha la wewe wa ndani mtu mwenye jicho la uovu anakuwa na roho chafu za kishetani zinakaa ndani yake kikutazama unapatwa na mabaya sababu ya roho chafu zilizo ndani yake.
Miaka mingi iliyopit nilipata uzoefu flani, siku moja tulikua na mkesha wa maombi ya kuwafungua watu lakini jambo la ajabu likatokea usiku ule.
Kukatokea watu ambao ni watu wa kanisani.
Mmoja wao akapandisha mashetani akasema tuko hapa leo na tumekuja kwa kazi maalumu na mwingine akaitikia ndio tupo na akatokea wa tatu naye akasema tuko hapa leo na tumekuja kwa kazi maaumu na mwingine akaitikia ndio tupo na akatokea wa tatu naye akasema ndio tupo kwa ajili ya kazi maalumu japo hawakuwa wanajuana kimwili lakini rohoni walitambuana na kusudi lao.

Ikawa ni ajabu. Wale watu watatu wakasema tupige mionzi ikawa wakimtazama mtu, mtu analala chini usingizi baada ya dakika tatu, watu wote wakawa wameanguka chini wamelala ni kabaki mimi peke yangu na wakaambizana tummalize na huyu anayejifanya kimbele mbele.

Wakasema wanigeukie na mimi huku macho yao yanatoa mionzi waliponigeukia mimi nikashangaa nguvu zinaniishia huku wao wanacheka na ni watu ninaowafahamu ni wa kanisani siku zote wanasali na kukesha lakini wamegeuka ghafla na kuanza kutenda hayo.

Wakaona nimechoka sana, ikabidi nijfiche , " kujificha ni moja ya silaha ya kiroho, hata Daudi wakati anakimbizwa na sauli alikimbilia akajificha kwa wafilisti.

Wafilisti walipomuona wakamtambua kuwa ni yule daudi aliyemuua Goliati ikabidi daudi ajifanye kichaa mpaka wakashindwa kumuelewa wakamwacha akaenda zake maana walijua mtu kama daudi hakuwa chizi"  kuna wakati wa kujificha ili kuepuka vita Fulani ipite uiangalie kama unaweza kuikabili kwa muda upi ndipo upambane nayo.

Ikabidi niondoke niende nyumbani nikaingia kwenye gari nikaelekea nyumbani nikafika nyumbani nikaingia nyumbani ni kamwambia mke wangu aniombee huku nimelala sababu nikuwa nimezidiwa sana sina nguvu mke wangu akaendelea kuniombea, Nikajiuliza kuwa mtumishi wa mungu ndio inakuwa hatari namna hii je wengine yanawapata kama haya yaliyonipata mimi ??

Baadaye mungu akaniambia mwanadamu ni roho inayokaa ndani ya nyumba inayoitwa mwili.
Ndipo nika tambua kuna watu wanaoingiwa na mashetani kwenye miili yao na kutenda kazi za kuharibu maisha ya watu kwa kutumia macho yao, hao tunawashughulikia kwa kina la yesu kristo
Kuna siku za kujificha na kuna siku za kushushwa kwenye kikapu.
Kila jambo na wakati wake ukifika wakati wa kuwekwa kwenye kikapu unatulia kuna mambo mengine sio ya kukabiliana nayo mara myanapo jitokeza unapisha yanapita yaende zake.
Mungu akitaka kuleta wokovu anatengeneza mazingira kwanza
Wakati ule ndio ulikuwa umerudishwa msukule kwa mara ya kwanza na ilikuwa tukiacha kuomba anamchukuliwa tena na mimi nilikuwa sijalala siku tatu na kesha na kumuombea mtu yale.
Siku ya tatu nikawaaombea na wasimwache alale waendelee kuomba maana wakinyamaza tu anachukuliwa tena.
Na kumbe aliyemchukua mtu msukule alikuwepo na ni mtu wa knisani alikua anafundisha watoto wadogo darasa na usiku ule alikuepobkwenye ule mkesha.
Ukitaka kuliangusha jengo angalia msingi usiwaze tu kuwa unaweza kwa kazi hii ukishinda kuzimu ukashinda na mauti umeshinda ufalme wa shetani wote.
Nataka nikuambie wewe sio wewe unayeonekana mwili wako, wewe ni yule wa ndani macho yako ni madirisha ya mtu wa ndani yako.
Kuna watu wapo lakini wana jicho ovu, mungu akaniambia roho za watu hawa zimetolewa ndani yao na shetani mwenyewe ameingia ndani ya miili yao ndio anakushambulia kwa jicho
Jioni ile kulikuwa na ibada nikamwambia mchungaji wangu waite wale kinadada watatu wafungie ndani, kuna waite wale kina dada watatu wafungie ndani, kuna wakati wa kukimbia ndio maana yesu alipozaliwa ktk Bethelehemu ya uyahudi mungu alimwambia yusuphu mchukue mtoto na mama yake mkimbilie Nazareti maana Herode anataka kumuua mtoto.
Japo alikuwa mungu lakini aliamua kukimbia sababu ulikua ni wakati

Baada ya ibada nikamwambia mchungaji yule wafungulie watoke wanacheka waanza kurusha tena ile mionzi
Ni kasema naamuru mionzi iwarudie wenyewe kwa jina la yesu.
Mionzi ikaanza kuwarudia wao wenyewe wakagalagala chini baadaye wakaombewa.
Duniani kuna macho ya uharibifu yakikupiga uharibifu unakupata lakini leo tutayapiga macho ya uovu.
Kuna wengine ukiwaangalia tu lzima uwafate unatekwa ufahamu wako unajikuta unawasemesha kwa ajili ya macho yao ya uovu wanakuchukua na kukupeleka pabaya.
Mungu ni roho lakini ana macho, ana miguu.
Na haya macho ya uovu sio kwamba mtu ametaka ni kwamba kwenye kila familia kuna makulani wa familia wa kichawi, mtu wa familia kukuloga ni rahisi kwa sababu najua vizuri ukoo wenu na akiwa anakaribia kufa unakuta anamkabidhi mtu mwingine mikoba yake
Unakuta mtu aliyeachiwa mkoba ana okoka na mikoba yake kwa hiyo unajikuta una macho ya uovu bila wewe kujua na mtu mwenye macho ya uovu sio lazima akuangalie ndio upatwe na matatizo.
Kuna mtu ameimaliza familia yake yeye mwenyewe, kuna mtu mwenye macho ya kichawi akiangalia biashara lazima ufunge.
Inawezekana ugonjwa ulio nao au taabu ulionao ni mtu alikuangalia akaachilia uovu kupitia macho yake.

Ktk jina la yesu naaguza macho ya ubaya yang'oke ndani yangu kwa jina damu ya mwana kondoo amen

Matatizo yana chanzo chake
Kila tatizo liwe la ndoa au la kibiashara au la kazi lina chanzo chake moja kati ya chanzo cha tatizo ni jicho ovu.
Unaweza ukawa unapata matatizo mara kwa mara kwa sababu kuna mtu anakuja kwako kukutazama na kukuletea matatizo mara kwa mara
( Tatizo halikupati mpaka kuwe na wakala wa kusababisha tatizo hilo )

Kwa kawaida mwanadamu ana milango mitano ya fahamu ambayo ni macho pua, ulimi, masikio, lakini wachawi wana mlango mwingine wa fahamu ambao ni mlango wa sila ambao wanautumia kufanya mambo yao ( waefeso 6:12 )

Hakuna kitu chenge nguvu kama maarifa ya rohoni, ukiomba vinzuri ukarudisha mishale ya wale wanaokurushia asubuhi mapema kabla hujatoka nyumbani siku yako itakua salama na ya ushindi kwa jina la yesu ( yohana 1:12 ) sisi ni wana wa mungu tukisema jambo lazima liwe ( ufunuo wa yohana 19:11,13 )
Tukisema neno kwa jina la yesu kuna vitu vinafanyika vya ushindi, unaposema neno lolote maana yake ni mungu anasema mungu na ndani ya nyumba kuna vitu vingi vinaweza kukaa.

Kifo si kitu lakini ni utengano ni sawa na mtu unapotoka ndani ya nyumba ukitoka kunakuwa na utengano wewe na nyumba yako na hufufuka ni kurudishwa ndani ya nyumba yako iutwayo mwili, kuna mtu mwingine ana majini anatuma yaingie kwenye sura yako ili ukose upendeleo

Wewe umeubwa kwa sura ya mungu, yale ambayo mungu anakusikia ukisema ndiyo ambayo atakutendea
Kwa jina yesu mtu ye yote aliyetuma mishale laana, mauti, umasikini, magonjwa au nisiyemjua aliyerusha mishale kwenye maisha yangu namrudiahia yeye kwa jina la yesu ( ufunuo wa yohana 1:10 )

Unaweza ukawa na tatizo lakini kila ukiomba kuna mtu anakuja kukutembelea tena ili aongezee lileitatizo unachotakiwa kufanya ni kuomba mambo ya mungu huwa ni kawaida sababu yanafanyika kwa kusema tu mungu ni msemaji sababu aliumba dunia.
Mashetani wanafahamu kesho utakuwa nani.
Hivyo ameaema utakuwa. Unatakiwa uone kuwa siku zijazo utakuwa mtu wa aina gani kama huoni basi kuna tatizo hapo.
Kila mwenye tatizo lililotokana na jicho la uovu haribu na uwarudishe wao wenye kwa jina la yesu Amen

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Jinsi ya kutengeneza sabuni ya maji

Jinsi ya kutengeneza sabuni ya maji Malighafi: 1. Sulphonic Acid Lt 2 2. Soda Ash Kg 1 3. Sless Lt 1 4. Chumvi Kg 1 5. Pafyumu /rangi Bluu 6. Maji Lt 35 _ 40 Jinsi ya kutangeneza Anza kwa kuweka lita 10 mara tatu, yaani lita 10 tena na mwisho lita 10, angalia uzito ongeza tena lita 5 na kisha lita 2 ikiwa uzito bado ongeza lita 2 na mwisho lita 1 4. Chumvi kg 1 3. Sless Lt 1 2. Soda Ash Kg1 1. Sulphonics Acid Lt 2 Hapo sijaweka rangi wala pafyumu kwa sababu ukiweka pafyumu lita 35 bila kufunika itaisha baada ya muda mfupi. Ni vema rangi na pafyumu uweke pembeni. Mfano: Chukua ndoo ya lita 10, weka rangi robo kijiko cha chai na pafyumu vijiko vya chakula viwili na koroga vizuri. Ni vema utumie pafyumu aina ya lemon. Sababu za kutoweka rangi sabuni yote: Wapo wateja hawapendi rangi na harufu kwa hiyo utawapa kila mtu kama atakavyo na kujaza kwenye chupa zako zenye mifuniko saa hiyo hiyo ukiachia muda inatoka harufu. Asante sana rafiki.

Fahamu jinsi ya kutengeneza sabuni ya vyoo

Sabuni ya kusafisha vyoo Malighafi. 1. Sulphonics Acid Lita 1 2. Soda Ash nusu 1/2 kilo 3. Sless 4. Chumvi 1/2 kilo 5. Maji lita 17 1/2 _ 20 6. Rangi kijani 7. Pafyumu 8. Formalin Jinsi ya kutengeneza Weka maji lita 5 kisha anza kukoroga, ongeza lita 5 kisha lita 5 tena na mwisho lita 2 4. Chumvi 1/2 kg 3. Sless nusu lita 2. Soda ash nusu kilo 1. Sulphonics Acid lita 1 Hapo sijaweka rangi wala pafyumu ni vinzuri kuweka kwenye ndoo lita 10 ya sabuni utaweka rangi kijiko 1 cha chai, rangi ya kijani pafyumu aina ya ' Rose two one ' au pino vijiko 5 vya chakula na Formalin vijiko 3 vya chakula. Formalin kwa ajili ya kuua wadudu ( bacteria ) ni vinzuri sana kuwemo kwenye sabuni ya chooni kwani ina kazi nyingi zaidi ya hiyo iliyotajwa Asante sana rafiki sasa chukua hatua ya kufanya hakika utafanikiwa sana

Somo: Roho mtakatifu Na mwl Christopher Mwakasege

Kushirikiana Na Roho Mtakatifu Anapotumia Moto kukuongoza ili utembee kwenye mapenzi ya mungu Biblia inafundisha ya kuwa wana wa mungu huwa wanaishi na wanatakiwa waishi kwa kuongozwa na roho mtakatifu ( warumi 8 : 14, 16, 17 ) Njia moja wapo anayotumia roho Mtakatifu kumwongoza mwana wa mungu, ni kwa kutumia moto wa mungu anaokuja nao ndani ya mtu anapoingia kukaa kwake Biblia inasema juu ya yesu ya kuwa yeye atawabatiza kwa roho mtakatifu na kwa moto ( luka 3 : 16 ) na siku ya pentekoste, wakati wanafunzi wa kwanza wa yesu, walipokuwa wamekutanika pamoja kukuwatokea ndimi zilizogawanyika, kama ndimi za moto uliowakalia kila mmoja wao wote wakajazwa roho mtakatifu ( matendo 2 : 3,4 ) Unaposoma na kutafakari jambo lililotokea siku hiyo ya pentekoste, utajua kuwa kuna uhusiano kati ya ndimi za moto juu ya kila mmoja wao na kule kujazwa roho mtakatifu kwa kila mmoja wao ni dhahiri ya kuwa roho mtakatifu anaingia ndani ya kila mwana wa mungu akiwa pia na moto wa mungu pamoja nao kazi m...