Harusi ni sherehe ndefu, kuna mambo mengi ambayo hufanyika ktk kipindi hiki muhimu hususani kwa wanandia.
Kila mmoja huwa ana majukumu yake ktk kuhakikisha sherehe inafabyika kwa ukamilifu.
Haya hapa ni baadhi ya majukumu ya msingi kwa bibu harusi.
Tumia vizuri wapambe wako
Waombe wakufuatilie kwa karibu hasa kwenye sherehe ili usitumie muda nwingi kuzungumza na wageni au mgeni mmoja, lakini kujua mahitaji yako siku hiyo muhimu.
Piga picha kabla ya kuanza kwa sherehe
Zipo faida kadhaa za kufanya jambo hili kwanza kabla ya kuendelea kwa sherehe.
Kubwa zaidi ni kupata mapambo halisi ya bibi harusi kabla hajachoshwa na muzunguko.
Hata kama picha nyingine zitafutia. Lakini hizi za mwanzo huwa na mvuto zaidi.
Kuwa huru na mavazi yako
Hakikisha unavaa kile kinachokuweka huru. Vaa viatu vinavyokutosha, vaa gauni linalokukaa vizuri.
Hii itakufanya uwe na raha muda wote, kwani ule wasiwasi wa kudhani hauko sawa utakuwa haupo.
Mara nyingi haya huchangia kumfanya bi harusi asiwe na utulivu.
Usisahau kula
Hakikisha unakula chakula cha asubuhi cha kutosha. Pia si vibaya kubeba vitafunwa vya kiba endapo utasikia njaa
Weka mbali simu yako
Wakati mwingine simu inaweza kukuchanganya. Ni vyema ukaiweka mbali ili kujikita zaidi na mambo ya harusi
Hakikisha unakuwa wa kwanza
Kumbuka hii ni siku yako. Hivyo hakikisha furaha yako inakuwa jambo muhimu sana.
Unatakiwa kujitanguliza kwa kila kitu. Ni siku yako na haitakuja mara ya pili
Fahamu mazingira ya eneo uliopo
Pamoja na kuwa na wasaidizi, ni vyema ukaelewa eneo ulilopo na kuongeza umakini.
Kwa mfano unapotembea ni vizuri kufahamu eneo lina ngazi ama kuteleza
Furahia
Ni siku yako, na watu wote walioko mbele yako wamekufuata wewe. Onyesha furaha.
Asante sana
Maoni
Chapisha Maoni