Kwa ufupisho, Biblia inasema kwamba wafu wako kaburini wakingojea ufufuo. ( yohana 5: 28, 29 ) inasema hivi "Msistaajabie maneno hayo; kwa maana saa yaja,ambayo watu wote waliomo makaburini watasikia sauti yake Nao watatoka; wale waliofanya mema kwa ufufuo wa uzima, na wale waliotenda mabaya kwa ufufuo wa hukumu." Hawateseki au kuhisi maumivu yoyote, kwa sababu " wafu, hawajui lolote kamwe." ( mhubiri 9: 5 ) inasema hivi "kwa sababu walio hai wanajua ya kwamba watakufa; lakini wafu hawajui neno lolote , wala hawana ijara tena; maana kumbukumbu lao limesahuliwa." katika mafundisho yake, Yesu alilinganisha kifo na usingizi mzito. ( yohana 11: 11- 14 ) Hivyo basi, Hatuna sababu yoyote ya kuwaogopa wale waliokufa au kuwatuliza kwa kuwatolea vitu mbalimbali. Hawawezi kutusaidia wala kutudhuru, kwa sababu " Hakuna kazi, wala utungaji wala ujuzi wala hekima ktk kaburi." ( Mhubiri 9: 10 ) Hata hivyo, kupitia ufufuo, Mungu atakishinsa kifo milele. ( 1 wakorintho 15: 26 ) inasema hivi " Adui wa mwisho atakayebatilishwa ni mauti na 55 inasema hivi " Ku wapi, Ewe mauti, Uchungu wako
HAKUNA ANDIKO KATIKA BIBLIA LINALOTAJA KUHUSU " NAFSI ISIYOWEZA KUFA"
Ki ya kati, Wanafalsafa Wagiriki walikuwa wameeneza fundisho hilo, na muda mfupi baadaye, lilienea ktk Milki yote ya Ugiriki. Katika karne ya kwanza W. K ., Madhehebu mawili maarufu ya kiyahudi, ambayo ni waesene na mafarisayo, yalifundisha kwamba nafsi huendelea kuishi baada ya mwili kufa . kitabu The jewish Encyclopedia Kinasema : " Fundisho la kutokufa kwa nafsi liliwafikia Wayahudi baada ya kuanza kupokea mawazo ya Wagiriki hasa kupitia falsafa ya Plato." Vivyo hivyo, Josephus, mwanahistoria Myahudi wa karne ya kwanza alisema fundisho hilo halitokani na maandiko matakatifu, bali linatokana na " imani ya wana wa Ugiriki ", Aliyoiona kuwa mkusanyo wa hekayo zao. Kadiri tamaduni za Wagiriki zilivyoenea, watu waliodai kuwa Wakristo walianza pia kukubali fundiaho hilo la kipagani. Kulingana na mwanahistoria Jona Lendering, " Ilikuwa rahisi kuunganisha falsafa ya Plato kwamba mwanzoni nafsi zetu zilikuwa mahali pazuri na sasa zinaishi ulimwengu uliopotoka." Hivyo, fundisho la kipagani kuhusu kutokufa kwa nafsi likapenya katika kanisa la " kikristo " na kuwa sehemu kuu ya imani yake.
Maoni
Chapisha Maoni