1: Utengenezaji wa sabuni za mche
Malighafi:
1: Caustic kg 4
2: Maji lita 10
3: Mafuta lita 20
4: Sodium Silicate Kg 2
5: pafyumu mili lita. 250 __ 300
6: Chumvi vijiko 2 vikubwa
Sabuni hii unaweza kuogea na kufulia inakuwa nzuri sana.
Jinsi ya kutengeneza
Loweka Caustic kg 4 kwenye maji ya lita 10 kwa siku 3. Ndani ya siku hizo tatu, utakuwa ukikoroga kila siku asubuhi na jioni kwa dakika 5. Kisha chukua sodium silicate kg2 ikifuatiwa na chumvi vijiko 2 vya chakula na mafuta huku unaendelea kukoroga kwa juhudi.
Baada ya hapo weka kwenye maumbo kwa siku 3 __ 5 ili igande vizuri.
Asante sana rafiki
Maoni
Chapisha Maoni