Kijiti kilichowaka moto ili mungu apate utayari na usikivu wa moyo wa musa ktk kile alichotaka kuzungumza naye wakati ule
Musa alikuwa anaendelea na kazi ya kuchunga kundi la kondoo la baba mkwe wake wakati alipoona mwali wa moto uliotoka katikati ya kijiti akatazama na kumbe kile kijiti kiliwaka moto nacho kijiti hakikuteketea ( kutoka 3:2 )
Ukiifatilia habari hii kwa makini utaona ya kuwa mungu hakujifunua na kusemabna musa hadi musa alipogeuka kutoka kujua kwa nini kijiti hakiteketei, ingawa kilikuwa kinawaka moto na musa alipogeuka na Bwana alipoona ya kuwa amegeuka ili atazame mungu akamwita kutoka katikati ya kile kijiti akasema musa musa akasema mimi hapa ( kutoka 3:4 ) mungu lizungumza mambo kadha wa kadha kabla musa hajakubali kuupokea na kuutekeleza wito aliyoitiwa, utayapata mambo hayo ( kutoka 3,4,22 ) na ( kutoka 4,1,29 )
Ninachotaka tujifunze hapa si ile hatua ya mungu ya kujifunua na kusema na musa Ninachotaka tujifunze katika habari hii ni kutoka kujua juu ya sababu iliyomfanya mungu ajifunue jinsi alivyojifunua yaani ya kutumia moto, sababu hiyo tunaipata tunaposoma maneno ambayo mungu alisema na musa mara tu baada ya musa kuitika alipoitwa jina lake Biblia inatueleza maneno ambayo mungu aliyasema kutoka katikati ya kijiti kilichokuwa kinawaka moto lakini bila kuteketea mungu alimwambia musa hii usikaribie hapa vua viatu vya miguuni mwako maana mahali hapa unaposimama ni nchi takatifu ( kutoka 3:5 )
Mungu alikuwa ana maana gani alipomwambia musa hivi vua viatu vyako miguuni mwako kufuatana na ( waefeso 6: ) miguu huwa inabebeshwa jukumu la kuchukua utayari wa kutumwa kupeleka habari muhimu mahali inapotakiwa kupelekwa wakati ule mungu alipotakiwa kupelekwa wakati ule mungu alipokuwa anazungumza na musa miguu ya musa ilikuwa imebebaa utayari wa kutumwa na baba mkwe wake aliyeitwa yethro kwenda kuchunga kundi lake la mifugo na inaonekana wazi ya kuwa mungu aliona ya kuwa viatu alivyovaa musa au utayari aliokuwa nao musa wa kumsikiliza Baba mkwe wake kwa wakati ule usingempa usikivu wa kutosha wa kusikiliza kile ambacho mungu alitaka kusema naye
Mungu hakujifunua kwa musa wala kumpa maelekezo yaliyohusu wito wake hadi musa alipovua viatu vyake kwa hiyo tunaweza kusema mungu alijifunua kwa kutumia moto kwenye kijiti ili apte utayari na usikivu wa moyo wa musa ktk kile alichotaka kuzungumza naye wakati ule kumbuka Agano la kale lilifungwa kwa mwili au kwa mtu kutahiriwa kwa jinsi ya mwili lakini Agano jipya lilifungwa na linafungwa kwa mtu kutahiriwa moyo wake kwa jinsi ya rohoni kwa mantiki hii ina maana ktk agano jipya moto wa roho mtakatifu ambao mungu atatuweka miyoni mwetu wakati anataka mioyo yetu iwe na utayari na usikivu kwake kwa hiyo wakati mwingine unaposikia moto unawaka moyoni mwako Bila kuzimika ujue kuna uwezokano mkubwa kuwa mungu anatafuta utayari na usikivu wa moyo wako ktk kile anachotaka kukueleza moto kwenye kijiti uliambatana na kile ambacho mungu alitaka asikie lakini baada ya musa kugeuka na kuitika kwa hiyo unaposikia moto moyoni mwako mwambie mungu kwa njia maombi ya kuwa umegeuka na uko tayari kumsikiliza naamini mungu atakusemesha kile alichotaka usikie kutoka kwake
Maoni
Chapisha Maoni