Njisi Roho Mtakatifu Anavyomuongoza Mtu Kwa Kutumia Moto Wa Mungu
Moto wa mungu unapowaka ndani ya moyo wa mtu wakati mtu huyo anapokuwa ktk mazingira yanayompa hasira au yanampa kukata tamaa, Na kwa ajili hiyo Roho Mtakatifu anawezka hiyo ishara ya moto wa mungu ndani ya moyo wa mtu huyo ili kumwonya ajizuie mungu ndani ya moyo wa mtu huyo ili kumwonya ajizuie kusema maneno yatakayofanya hali yake ikawa mbaya zaidi.
Jaribu kubwa kwa mtu yeyote anayepitia kwenye mazingira magumu au mazingira yaliyo kinyume na matarajio yake ni kule kutakabkusema maneno yaliyo jaa hasira au yaliyo jaa kukata tamaa.
Biblia inatueleza ya kuwa mungu aliwaongoza wana wa israeli ktk safari yao ya kutoka misri na kwenda kaanani kwa wingu wakati wa mchana na kwa moto wakati wa usiku ( hesabu 14:14 )
Wingu wakati wa mchana na moto wakati wa usiku, vilikuwa ni ishara ya uwepo wa uongozi wa Roho Mtakatifu kwa ajili yao wakati wote yaani mchana na usiku ishara zote hizi mbili zilikuwa zinaonekana kwa macho wa mwili kwa sababu agano lao mungu lilifugwa kwa ishara ya tohara ya mwili ( mwanzo 17:11,13 )
Wakati huu wa kipindi cha agano jipya ishara ya kuwa ni haki yako kuongozwa na roho mtakatifu wakati wote yaani mchana na usiku ni mtu kutahiriwa moyo wake ( warumi 2:29 ) ingawa mungu bado anaweza kutumia wingu na moto kuongoza watu wake akitaka.
Lakini kwenye kipindi hiki cha agano jipya mara nyingi na kwa sehemu kubwa anamuongoza mtu toka ndani ya moyo wake kwa kutumia Roho Mtakatifu aluyeingia ndani yake siku ile alipookoka.
Mazingirabya safari ya wana wa israeli kutoka misri kwenda kaanani haya kuwa mepesi mara nyingi walikutana na mzaingira magumu na ya kukatisha tamaa.
Kwa jinsi ya kibinadamu na wakajikuta wanasema maneno ambayo yalionyesha ya kuwa wamesahau ukuu wa mungu aliyekuwa pamoja nao wakati wote katika safari yao ingawa mungu alikuwa mvumilivu sana kwao walipokuwa wanasema maneno magumu na yakukata tamaa wakiwa ktk uwepo wake na chini ya uongozi wake.
Lakini hakuwa mvumilivu hivyo kwa wakati wote wakati mwingine aliwakasirikia sana aliposikia maneno waliyo yasema kiasi cha kuwaacha waingie ktk shida.
Je unakumbuka wana wa israeli walisema nini walipotetewa habari mbaya na wale wapelelezi kumi waliotumwa ili kuipeleleza nchi ya kaanani.
Biblia inasema wote wakamnungunikia musa na Haruni wakwaambia, ingekuwa heri kama tungalikufa ktk jangwa hili, mbona Bwana anatuleta mpaka nchi hii ili tuanguke kwa upanga wake zetu na watoto wetu watakuwa mateka je si afadhari turudi misri ( hesabu 14:2,3 )
Maneno hayo haya kumfurahisha mungu alipoyasikia kumbuka.
Mungu alikuwa anajua ya kuwa hali iliyowafanya wanung'unike na kukata tamaa ya kuendelea na safari yao na Bwana ilikuwa halisi na mazingira yalikuwa halisi pia.
Lakini maneno waliyoyasema ktk mazingira yale yalipeleka ujumbe uliokuwa mbaya masikioni mwa mungu wao.
Bwana akamwuliza musa je watu hawa watanidharau hata lini wasiniamini hata lini.
Ni japo kuwa nimefanya ishara hizi zote kati yao ( hesabu 14:11 )
Mungu akaendelea kusema hivi je ni chukuane na mkutano mwovu huu unung'unikiao.
Kama niishivyo, asema Bwana hakika yangu kama ninyi nilivyonena masikioni mwangu ndivyo nitakavyowafanyia ninyi ( hesabu 14:27,28 )
Na kw sababu hii ya kuonyesha kutokuamini kwao kwa njia ya maneno waliyo yasema walifia jagwani ukiifutilia vinzuri habari hii, utaona ya kuwa katikati ya manung'uniko yale na hasira walioonyesha juu ya yoshua na kalebu na musa na haruni.
Utukufu wa Bwana ukaonekana ktk hema la kukutania mbele ya wana wa israeli wote ( hesabu 14:10 )
Wakati wa kipindi hiki cha agano jipya mara nyingi utukufu wa Bwana unaonekana kwa ishara ya moto moyoni mwa mtu kabla hajasema maneno yatakayo sababisha akwame zaidi.
Tunaposema ( yakobo 3:5,6,9,10 ) tunaona kuwa
Ulimi nao ni kiungo kidogo, nao hujivuna majivuno makuu.
Angalieni jinsi moto mdogo uwashavyo msitu mkubwa sana na ulimi ni moto kwa huo twamhimidi mungu Baba yetu na kwa huo twawa laani wanadamu waliofanywa kwa mfano wa mungu ktk kinywa kile kile hutoka baraka na laana.
Ndugu zangu haifai mambo hayo kuwa hivyo.
Ni dhahiri kwamba kwa kuwa mungu hataki uwashe moto kwa kinywa chako utakaoleta shida kwako na kwa wale wanaokuzunguka anakuwekea ishara ya moto wake moyoni mwako unapopitia hali ngumu ili kukupa onyo uchunge na uzuie kinywa chako na ulimi wako usije ukasema maneno yatakayowasha moto utakaosababisha ukwame zaidi.
Mazingira ya namna hii yanapotokea kwako utaona.
Biblia inashauri yafuatayo
1: omba mungu awe anakuwekea mlinzi au ulinzi kwenye kinywa chako ili usiwe unasema maneno yasiyofaa masikioni mwa mingu hata kama unapita ktk mazingira magumu ( zaburi 39:1,3 ) ( zaburi 14:1,3 )
2: Jitahidi kuka kimya bila kujibu au kujibizana maana biblia insema laiti mngenyamaza kabisa hilo lingekuwa hekima kwenu ( ayubu 13:5 )
3: Tafakari na kuombea ahadi ya mungu iliyopo ktk neno lake inayozungumzia juu ya jibu la mungu ktk kutatua tatizo hilo
4: Ikiwa huna neno la namna hiyo, basi tafakari shuhuda za mungu zilizomo ktk Biblia na ulizozisikia ktk maisha ya watu zinazoonyesha ukuu, na uweza na utayari wa mungu ktk kutatua matatizo kama uliyonayo
5: usimdharau au kumkosea mungu kwa kinywa chako ikiwa unjua umemkosea basi tubu juu ya hilo Ayabu alipikuwa anapitia hali ngumu ya maisha Biblia inasema ktk mambo hayo yote Ayubu hakuganya dhambi kwa midomo yake ( ayubu 2: 10 )
6: kila upatapo nafasi na hata kama akili zako zinakubishia endelea kukiri na kushikilia ahadi za mungu na uaminifu wa mungu naye atafanya ( warumi 4:20,21 ) na kumbuka rehema zake ni mpya kila asubuhi ili tusingamie ( maombolezo 3,22,23 )
Maoni
Chapisha Maoni