Jinsi Roho Mtakatifu Anavyotumia Moto Wa Mungu Ktk Kuongoza Mtu
Moto ndani yako kama ishara ya roho mtakatifu kukuhimiza usiache kufanya kile ambacho amekuingiza ukifanye, hata kama upinzani dhidi yako ni mkubwa ili usikifanye.
Nabii yeremia alikutana na hali ya namna hii, wakati wa kipindi alipokutana na upinzani dhidi ya utumishi aliokuwa amepewa na mungu upinzani huo ulimfikisha mahali pa kuona ya kwamba amekuwa kitu cha kuchekesha mchana kutwa ( yeremia 20:7 )
Nabii yeremia aliona kama vile neno la bwana limefanywa shutumu na dhihaka kwake mchana kutwa ( yeremia 20: 8 ) na kwa sababu hiyo anasema nami sitamtaja wala sitasema tena kwa jina lake ( yeremia 20: 9 ) kwa tafsiri nyingine upinzani dhidi ya utumishi aliopewa na mungu ulimfikisha mahali pa kuamua kutokusema tena kwa jina la mungu wala asimtaje mungu popote tena uamuzi huo haukumfanya mungu anyamaze bila kufanya jambo lililomwonyesha nabii yeremia ya kuwa mungu hakukubaliana n uamuzi wake ule.
Nabii yeremia anaeleza yaliyotokea hii nami nikisema sitamtaja wala sitasema tena kwa jina lake basi ndio moyoni mwangu kumekuwamo kama moto uwakao uliofungwa ndani ya mifupa yangu, nami siwezi kustahimili, wala siwezi kujizuia ( yeremia 20:9 )
Kwa tafsiri nyingine nabii yeremia alitaka tujue ya kuwa alipoamua kuacha kufanya alichotumwa na mungu kwa sababu ya upinzani dhidi yake.
Mungu aliwasha moto ndani yake ambao aliona kama vile umefungwa ndani ya mifupa yake na ujumbe wa mungu ktk moto ule ulikuwa ni wakumhimiza yeremia abadili msimamo wake wa kuacha kufanya kazi aliyopewa na mungu na badala yake aamue kuendelea kufanyabkazi kama alivyoelekezwa na mungu.
Hata katikati ya upinzani dhidi yake ukisoma vinzuri mstari huo, utaona ya kuwa yeremia hakukubali mapema kuufuata ujumbe wa mungu uliokuja kwake kwa njia ya ishara ya moto ndani yake ndio maana anasema juu ya moto ule ya kuwa nami siwezi kustahimili wala siwezi kustamili wala siwezi kujizuia.
Moto ule ulikuwa mkubwa sana moyoni mwake kiasi cha kuusikia ukiwaka na kufukuta kama vile umefungwa ndani ya mifupa yake.
Hali ile ya moto ule ilimfanya abadili uamuzi wake na akaamua aendelee kuifanya kazi aliyopewa aifanye na mungu.
Moto ule haukuja kumpa taarifa kuwa mungu atampa ushindi dhidi ya upinzani wake
Nabii yeremia anakiri kwa kinywa chake, juu ya ujumbe ulioingia moyoni mwake kwa njia ya moto wa mungu uliowaka ndani yake ya kuwa lakini bwana yu pamoja nami.
Mfano wa shujaa mwenye kutisha kwa hiyo hao wanaonionea watajikwaa, wala hawatashinda watatahayarika sana wataona aibu ya milele ambayo haitasauliwa kamwe ( yeremia 20:11 )
Kwa hiyo unapoacha au unaposikia kuendelea kuifanya kazi yabmungu uliyopewa kwa sababu ya upinzani dhidi yako unaokutana moyoni mwako moto huo moyoni mwako ni ishara ya roho mtakatifu ya kukupa ujumbe wa mungu kwako
____ Ya kuwa usiache kuifanya kazi ya mungu unayoifanya hata ikiwa umesongwa na upinzani mkubwa dhidi yako unaokukatisha tamaa usiendelee kuifanya
_____ Mungu yu pamoja nawe na atakupigania na kukupa ushindi dhidi ya upinzani uliokuandama
Ni maombi yangu kwa mungu kwamba anapokuwekea ishara ya moto wake moyoni mwako kwa njia Roho mtakatifu atakupa na ufafanuzi wake ili ujue moto huo una ujumbe gani wa kimaelekezo kwako kutoka kwake mungu. Amina
Maoni
Chapisha Maoni