Asili ya zao hili ni persia ulaya na kusini magharibi mwa Asia kwa Tanzania zao hili hulimwa hasa mikoa ya Iringa, mbeya, morogoro, Arusha na kilimanjaro
HALI YA HEWA & UDONGO
Karoti zinahitaji hali isiyokuwa na joto sana, wala baridi sana, kati ya nyuzi za degree 15 mpaka 27 za sentigredi. Kama ukanda wa pwani unajoto kali, inatakiwa karoti zilimwe miezi ya majira ya baridi, karoti zinazotoka mazingira ya baridi huwa na radha nzuri pamoja na harufu nzuri. Udongo wa kichanga chepesi na tifutifu ndio unafaa ktk kilimo cha karoti, udongo wa mfinyanzi na udongo mzito hudumaza mazao
UTAYALISHAJI WA SHAMBA
Karoti zinahitaji shamba lilimwe kwa trekta, kwa ng'ombe ama kwa jembe la mkono kwa kina cha sentimita 30 hadi 45. Mkulima anatakiwa kuandaa matuta yenye mwinuko wa kimo cha sentimita 28, 40 kwenye shamba na upana wa mita 1 pia mita 15 umbali wa tuta moja hadi lingine. Kwa maandalizi mazuri tengeneza mifereji midogo ya kusiha mbegu za karoti yenye umbali wa sentimita 15 - 20, mifereji minne kwa tuta.
UTATALISHAJI WA MBEGU
Jinsi ya kujua mbegu nzuri zenye uwezo wa kukua bila wasi wasi. mbegu zenye uwezo wa kuota hutoa harufu kali unapozifikisha. Zilizopoteza uwezo wa kuota huwa hazitoi harufu yoyote ili mbegu ziote haraka ziloweke ktk maji kwa muda wa saa 24 baada ya hapo changanya Mbengu hizo na mchanga, Kwa kiasi kinacholingana ili kupata mtawanyiko mzuri wa mbegu wakati wa kupanda
UPANDAJI
Ina hitaji uoteshe kwenye kitalu ndipo uhamishie shambani weka Mbegu ktk chupa ya milimita 100 na toboa kidogo mfuniko, baada ya hapo changanya Mbegu ktk mifereji ya kupanda kwa kutumia mboji au mchanga, ukimaliza myunyiza maji ya kutosha, funika tuta na plastiki nyeusi, hatua nyingine kandamiza plastiki kwa pembeni na kwa mabonge ya udongo ili isipeperushwe na upepo. Mbegu huota baada ya siku 3 - 5 kutegemea na hali ya hewa. Inakupasa kukagua shamba mara tatu kwa siku. Baadaye ondoa plastiki mara moja pindi utakapoona mbegu moja tu iliyoota. Usicheliweshe kuondoa plastiki husababisha miche inayoota kufa kwa kuunguzwa na joto lililo ktk plastiki. Hapo tayari kwa kupanda shambani upandaji wa moja kwa moja shambani ktk matuta au sesa kiasi cha kilo 8 za mbegu kinatosha kupandwa kwenye Hekta moja.
MBOLEA
Weka mbolea aina za asili ( Samadi au mboji ) mwanzoni, ila kama haukutumia mbolea ya samadi au mboji weka mbole ya S/A kilogramu 100 kwa hekta kama haukutumia mbolea ya asili, kama ulitumia mbolea za asili basi weka kilogramu 50 kwa hekta kisha tumia NPK wiki sita baada ya kupanda. Matumizi ya mbolea za maji yafanyike kila baada ya wiki mbili kutegemea na mahitaji
UPANDAJI & UNYEVU
Ili kupata mavuno mengi palilia shamba mara kwa mara ili kuhakikisha shamba halina magugu na nyasi kwa kung'olea kwa mkono, jembe na mangineyo, na kwenye udongo hakikisha kuna unyevu wa kutosha kama sio kipindi cha mvua inatakiwa umwagilie shamba lako kwa wiki mara mbili
Maoni
Chapisha Maoni