"Hakuna elementi iliyo muhimu zaidi ktk uhai kama kaboni," Kinaeleze kitabu Nature's Building Blocks. Muundo wa kaboni huiwezesha kuungana yenyewe na pia na kemikali nyingine nyingi, hivyo kufanyiza mamilioni ya miungano tata, na mingi kati ya miungano hiyo bado haijagunduliwa au kujulikana. Mifano ifuatayo inaonyeasha, jinsi atomu za kaboni zinavyoweza kuungana na kutokeza maumbo ya aina mbalimbali, kama vile minyororo, piramidi, pete, mabamba, na mirija. Kwa kweli, kaboni ni elementi ya ajabu
Kaboni___ Elementi inayotokana na Utendaji wa Nyota
Kaboni hutokana na miungano ya viini vitatu vya heliamu, ambavyo wanasayansi huamini kwamba vinapatikana ktk nyota kubwa ziitwazo majitu mekundu. Hata hivyo, ili heliamu ziungane, lazima hali fulani itokee kwa usahihi kabisa. Mwanafizikia Paul Davies alindika hivi: " Kubadili mambo machache tu [ katika sheria za asili ] Hata kwa kiasi kidogo sana, kungefanya kusiwepo ulimwengu, Uhai, Hata wanadamu." Tunajua jinsi gani kwamba hali hiyo hujitokeza yenyewe tu. Wengine huamini kwamba huo ni uthibitisho wa kuwapo kwa muumba mwenye hekima. Unafikiri ni maoni gani yaliyo sahihi?
ALMASI : Atomu za kaboni zinapoungana hutakeza piramidi ziitwazo tetrahedron, zilizo na umbo imara na hufanya almasi kiasili iwengumu kuliko kitu chochote. Kimsingi almasi halisi ni molekuli iliyofanuizwa na atomu za kaboni
GRAFITI : Ni tabak la atomu za kaboni zilizoungana na kujipanga kwa kuachiana nafasi kwa njia inayoweza kupekuliwa kama kurasa za kitabu. Kwa hiyo grafiti ni laini na ni muhimu katika utengezaji wa penseli. Ni tabaka moja la atomu za kaboni lenye mpangilio wenye matundu yenye umbo la penseli inaweza kuwa na kiasi kidogo cha grafati katika tabaka moja au zaidi
MOLEKULI ZA FULLERENE : Hizi ni molekuli za kaboni zenye mashimo na umbo la mviringo kama mpira na zingine zenye umbo la mirija zinazoitwa nanotube. Hupimwa katika nanometa, au mabilioni ya meta.
VIUMBE HAI : Chembe nyingi zinazofanuiza mimea, wanyama, na mwanadamu zinatokana na kaboni, yaani, elementi inayopatikana katika kabohaidreti, mafuta, na aminoasidi.
" Sifa za [ Mungu ] ambazo hazionekani.. Zinaeleweka kwa vitu vilivyofanywa." __ warumi 1: 20 inasema hivi " kwa sababu mambo yake yasiyoonekana tangu kuumbwa ulimwengu yanaonekana, na kufahamika kwa kazi zake; yaani, uweza wake wa milele na uungu wake; hata wasiwe na udhuru
Maoni
Chapisha Maoni