Dunia ni moja wapo ya sayari inayolea ktk anga ya ulimwengu. Kuna sayari nane zinazolizunguka jua, dunia yetu ikiwa sayari ya tatu ktk mfumo wa jua na sayari zake. Masafa baina yake na jua ni kilomita milioni 150 au kilio astronomia 1 dunia huchukua siku 365.256 kulizunguka jua, na masaa 23.9345 kuuzunguka mhimili wake na upana wake ni kilomita 12,756 dunia huwa na mwezi 1 umri wa dunia hukadiriwa kuwa miaka bilioni 4.5
UMBO LA DUNIA
Umbo la dunia linafanana na tufe au mpira unaozunguka kwenye mhimili wake. " Mhimili wa dunia " Ni mstari kati ya ncha zake. Lakini si tufe kamili. Ina uvimbe kidogo kwenye sehemu ya ikweta, ihali umbali kati ya sehemu za kinyume kwenye ikweta ni km 12,756, yaani kipenyo hiki kinazidi takriban kilomita 43 kipenyo kati ya ncha na ncha tofauti hii inasababishwa na mzunguko wa dunia kani nje inasukuma sehemu za ikweta nje zaidi. Kwa hiyo mahali dunia palipo karibu zaidi na anga la nje si mlima Everest kwenye himalaya bali mlimachimbarazo nchini Ekudor kwenye uso wake dunia huwa na tofauti kati ya nusutufe zake mbili nusu moja ina eneo kubwa la mabara yaani inchi kavu ambayo ni asilimia 47 ya sehemu hii kinyume nusutufe nyingine inafunikwa na maji ya bahari na eneo la nchi kavu ni asilimia ili pekee za maeneo yake. Kwa jumla dunia ni sayari pekee ktk mfumo wa jua yenye maji ktk hali ya kiowevu usoni mwake. Bahari kuu ya dunia inashika asilimia 96.5 ya maji yake yaliopo duniani maji ya bahari huwa na asilimia 3.5 chumvi ndani yake kwa pamoja maeneo ya maji hufunika 70.7% za uso wa dunia. Nchi kavu huwa na 29.3% na sehemu kubwa ya eneo la nchi kavu ni bara 7 za Asia, Afrika, Amerika kaskazini, Amerika kusini, Antarktika, ulaya na Australia ( Ulaya inaweza kuangaliwa pia kama sehemu ya Asia ikawa kama rasi yake ya magharibi. Azimio la kutazama Australia kama barua na Greenland kama kisiwa tu ni azimio la hiari si la lazima ) maeneo ya bahari kuu ya dunia kwa kawaida hugawiwa kwa bahari kubwa 3 za pasifiki, Atrantiki na bahari ya hindi. Sehemu ya chini baharini iko kwenye mfereji wa manana ktk pasifiki ( Mita 11, 034 chini ya UB ) kwa wastani bahari huwa na kina cha mita 3,800
Maoni
Chapisha Maoni