Leo tutakumbushana jambo hili la kujisomea, kwa nini kujisomea? Kujisomea ni ufahamu, kama huna ufahamu hutaweza kujisomea Ktk kujisomea tunatoa ujinga tunaingiza mahalifa, Tuna jenga akili ( Mathayo 22:29 ) nasoma kwa jina la Bwana, " yesu akajibu akawaambia, mwapotea, kwa kuwa hamyajui maandiko wala uweza wa mungu " Unapokosa kujisomea neno la mungu utakosa kujua uwezo wa mungu na nguvu zake, kila jambo kwako utakosa amani na imani na mungu wako. Naweza kusema hivi kuwa vitendo vya kukata viungo vya walemavu wa ngozi sababu ya kujipatia utajili ni imani potofu, Kwa maana hakuna mahali kwenye biblia palipo sema heti viungo vya walemavu wangozi vinzuri kwa kujipatia utajiri hakuna, hii ni imani potofu, sababu kubwa ni watu kutotaka kujisomea neno la mungu wanakosa ukweli wa mungu basi wanadanganyika na maneno ya shetani. Leo ninakupa ufahamu ili uweze kujisomea kwa maana faida ipo Je unamfahamu Daniel ? ( Daniel 9:12 ) inasema hivi " Ktk mwaka wa kwanza ...