Leo tutakumbushana jambo hili la kujisomea, kwa nini kujisomea?
Kujisomea ni ufahamu, kama huna ufahamu hutaweza kujisomea
Ktk kujisomea tunatoa ujinga tunaingiza mahalifa, Tuna jenga akili
( Mathayo 22:29 ) nasoma kwa jina la Bwana, " yesu akajibu akawaambia, mwapotea, kwa kuwa hamyajui maandiko wala uweza wa mungu "
Unapokosa kujisomea neno la mungu utakosa kujua uwezo wa mungu na nguvu zake, kila jambo kwako utakosa amani na imani na mungu wako.
Naweza kusema hivi kuwa vitendo vya kukata viungo vya walemavu wa ngozi sababu ya kujipatia utajili ni imani potofu,
Kwa maana hakuna mahali kwenye biblia palipo sema heti viungo vya walemavu wangozi vinzuri kwa kujipatia utajiri hakuna, hii ni imani potofu, sababu kubwa ni watu kutotaka kujisomea neno la mungu wanakosa ukweli wa mungu basi wanadanganyika na maneno ya shetani.
Leo ninakupa ufahamu ili uweze kujisomea kwa maana faida ipo Je unamfahamu Daniel ?
( Daniel 9:12 ) inasema hivi " Ktk mwaka wa kwanza wa Dario, mwana wa Ahasuero, wa uzao wamedi, aliyetawazwa kuwa mfalme juu ya milki ya wakaldayo ktk mwaka wa kwanza wa kumiliki kwake, mimi Daniel, kwa kuvisoma vitabu, nalifahamu hesabu ya miaka, ambayo neno la BWANA lilimjia yeremia nabii, ya kutimiza ukiwa wa yerusalemu, yaani, miaka sabini. "
Kumbuka nilikuwambia hivi, huwezi kujisomea kama huna ufahamu, Daniel alikuwa na ufahamu ya kujisomea vitabu ndipo akafahamu hesabu inayo wapasa kuka utumwani, kwa maana wana israeli walikuwa utumwani kipindi.
Ipo faida ktk kujisomea MUNGU HAKUPE UFAHAMU ILI UWEZE KUJISOMEA
Penda kujifunza ili akili yako iwe na matunda ndugu
Penda kujifunza ili akili yako iwe na matunda ndugu
Asante sana rafiki
Maoni
Chapisha Maoni