Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Mzigo wa magazeti ya Tanzania Sep 27, 2017

Chunguza Upya Viwango Na Malengo Yako

Ni kawaida kutamani kuwa na usalama wa kifedha kwa kiasi fulani. Lakini, ni kiwango kipi cha pesa kinachofaa? Mafanikio ni nini hasa? Je, yanapimwa kwa kutegemea tu kipato au mali za mtu? Kwa upande mwingine, kuwa na muda mwingi wa mapumziko au burudani kunaweza kuongeza mkazo. Tim, aliyenukuliwa awali anasema hivi: " mimi na mke wangu tulichunguza upya maisha yetu na kuamua kutarahisisha. Tulitengeneza chati iliyoonyesha hali yetu ya sasa na malengo yetu mapya. Tulizumgumza kuhusu matokeo ya maamuzi tuliyofanya zamani na kile tunachohitaji kufanya ili kufikia malengo yetu. Chukua maisha mapya ili kufikia malengo yako hacha kukumbuka nyuma ulipo toka. Kwa mafupi haya yafanyie kazi kwanza ndipo tu jifunze na kuangalia jambo lingine Asante sana rafiki msikivu

Teknolojia na Mkazo

Je, vifaa vya kisasa vya kielektroni huongeza u kupunguza mkazo unaotokana na kujisi kwamba tumebanwa na wakati? Jibu linategemea jinsi unavyotumia vifaa hivyo. Kazini: Simu za mkononi huwapa wtu uhuru wa kufanyi kazi mahali popote na muda wowote. Lakini zinaweza kuongeza mkazo kwa kufanya ionekane kwamba mtu anaweza kupatikana wakati wowote ule kwa ajili ya kazi iwe mchana u usiku. Nyumbani: Simu zinaweza kuwasaidia washiriki wa familia washirikiane kwa urahisi na hivyo kupunguza mkazo. Hata hivyo, zinaweza pua kuingilia wakati ambao familia inapaswa kutumia pamoja. Utafiti unaonyesha kwamba ikiwa watoto wanahisi wazazi wao huthamini zaidi vifaa vyao vya kielektroni, watakasirika na isiyo ya kawaida.

Umuhimu wa kupumua

Kila wakati tunapumua. Je ni lazima tupumue ? Hatuwezi tukakaa bila kupumua ? Tendo la 1: Kugundya ikiwa Tunaeza Kukaa Bila Kupumua Jaribu kutulia bila kuvuta hewa ndani. Umeweza kukaa bila kupumua kwa muda mrefu? Mtu akizuiwa kupumua anakufa. Hii ni kwa sababu mwili wake utakosa hewa. Je, hewa ina umuhimu gani ktk mwili? Chakula hutupatia nishati. Nishati hiyo hutuwezesha kufanya kazi. Vile vile nishati hiyo huuwezesha mwili kufanya kazi ndani yake ambayo ni ya lazima kwa uhai. Ili chakula kitupatie nishati ni lazima kibadilishwe. Mabadiliko hayo hayawezi kutokea ikiwa mwili utakosa hewa. Umuhimu wa maji Mwili wa mnyama siyo mkavu kama vile jiwe. Mwili una majimaji. Mifupa huonekana mikavu. Lakini kwa kweli ina kiasi fulani cha maji. Tukisikia kiu tunakunywa maji. Kiu ni ishara ya jambo gani? Tukisikia kiu maana yake maji yamepungua mwilini. Hivyo, kila wakati mwili unahitaji kuwa na maji kiasi fulani. Kwa nini mwili unahitaji maji ? Mwili ni lazima ufanye kazi zake...

Magonjwa Ya Kuambukiza

Magonjwa ya kuambukiza yapo ya aina nyingi. Magonjwa hayo huenezwa kwa njia mbalimbali. Ili kuzuia kuenea ni muhimu kuzingatia usafi wa mtu binafsi na wa mazingira. Magonjwa hayo ni kama vile, kuhara, kichocho, malaria, kuhara damu, homa ya matumbo na magonjwa ya ngozi, safura na minyoo. Kuhara Huu ni ugonjwa unaoletwa na vijidudu vinavyosababisha uvimbe wa tumbo. Ni ugonjwa wa kwenda haja kubwa mara nyingi kupita kiasi kwa siku moja Dalili .  Mgonjwa hujihisi msokoto wa tumbo .  Huenda haja kubwa laini sana mara nyingi kwa siku ( mara sita au zaidi ) .  ulimi huwa mkavu .  Wakati mwingine huweza kutapika. Ugonjwa unavyoenea Kuhara ni ugonjwa unaoenezwa kwa kunywa maji machafu. Pia mtu akila chakula kilichoguswa na inzi huweza kuharisha. Jinsi ya kujikinga na kuhara . ili kujikinga na ugonjwa wa kuhara zingatia mambo yafuatayo: .  kunywa maji safi na salama. .  Tumia choo kwa haja kubwa na ndogo .  Funika chakula ili inzi asiguse ....

Magazeti ya Tanzania sep26, 2017

Huduma ya kwanza kwa mtu aliyezirai

Hali ya mtubkuzirai inaweza kusababishwa na mambo yafuatayo; Maumivu makali. Ulegevu wa moyo. Habari za ghafla zilizo njema au mbaya. Kuona au kusikia mambo ya kuogofya. Uchovu kutokana na kusimama au kuketi kwa muda mrefu. mahali penye hewa nzito isiyo safi. kutokwa na damu kwa wingi. Mimba iliyotunga nje ya mhi wa uzazi na ugonjwa wa kisukari. Dalili za mtu aliyezirai .  Kupiga miayo kwa mfululizo .  kuona kizunguzungu .  kutokwa na jasho usoni, shingoni na mikononi .  Kupunguza upesi upesi na kuanza kupiteza na fahamu Huduma ya kwanza Mlaze chali mgonjwa. Legeza nguo zake zote, shingoni, kifuani na kiunoni. Mpatie mgonjwa hewa nyingi safi na zuia watu kusonga. Mpepee ili kumpatia hewa nyingi zaidi. Mnawishe uso wake kwa maji safi kama yanapatikana. Baada ya muda wa dakika 30 kupita bila matokeo, mpeleke mgonjwa zahanati. Hizi ni bahazi ila zinamanufaha kumpatia mgonjwa . Asante sana