Magonjwa ya kuambukiza yapo ya aina nyingi. Magonjwa hayo huenezwa kwa njia mbalimbali. Ili kuzuia kuenea ni muhimu kuzingatia usafi wa mtu binafsi na wa mazingira.
Magonjwa hayo ni kama vile, kuhara, kichocho, malaria, kuhara damu, homa ya matumbo na magonjwa ya ngozi, safura na minyoo.
Kuhara
Huu ni ugonjwa unaoletwa na vijidudu vinavyosababisha uvimbe wa tumbo. Ni ugonjwa wa kwenda haja kubwa mara nyingi kupita kiasi kwa siku moja
Dalili
. Mgonjwa hujihisi msokoto wa tumbo
. Huenda haja kubwa laini sana mara nyingi kwa siku ( mara sita au zaidi )
. ulimi huwa mkavu
. Wakati mwingine huweza kutapika.
Ugonjwa unavyoenea
Kuhara ni ugonjwa unaoenezwa kwa kunywa maji machafu.
Pia mtu akila chakula kilichoguswa na inzi huweza kuharisha.
Jinsi ya kujikinga na kuhara
. ili kujikinga na ugonjwa wa kuhara zingatia mambo yafuatayo:
. kunywa maji safi na salama.
. Tumia choo kwa haja kubwa na ndogo
. Funika chakula ili inzi asiguse
. Nawa mikono kwa sabuni kabla na baada ya kula.
. Safisha na menya matunda kabla ya kuyala
Leo nimekupa somo la ugonjwa mmoja wa kuhara, Ninakuahidi kukuletea magonjwa mengi na mengi hapa hapa msikuvu.blogspot.com
Usichoke kuwa pamoja nami asante sana
Maoni
Chapisha Maoni