Juma lililopita tulijifunza mpanda farasi wa rangi ya moto.
Tukajua kazi zake na mamlaka yake yote amepewa na nani? Sasa leo tunaendele na mpanda farasi mwingine nayeni MPANDAJI WA FARASI MWEUSI.
Tutajua kazi yake ni nini ? Ninakukaribisha rafiki yangu kuwa pamoja na mimi, karibu sana.
MPANDAJI WA FARASI MWEUSI
" Nami nikaona, na, tazama! Farasi mweusi, na yeye anayeketi juu yake alikuwa na mizani mkononi mwake. Nami nikasikia sauti kana kwamba ni katikati ya wale viumbe hai wanne ikisema: Kibaba cha ngano kwa dinari moja, na vibaba vitatu vya shayiri kwa dinari moja, na vibaba vitatu vya shayiri kwa dinari moja, wala usidhuru mafuta ya zeituni na divai." Ufunuo 6:5,6.
Mpanda farasi huyo anawakilisha njaa. Njaa imekithiri hivi kwamba kibaba cha ngano kinagharimu dinari moja, yaani, mshahara wa siku moja ktk karne ya kwanza! ( Mathayo 20:2 ) Dinari hiyo pia ingeweza kununua vibaba vitatu vya shayiri, nafaka ambayo haikuonwa bora kama ngano. Je kiasi hicho kingetosha familia kubwa? Kisha, watu wanaonywa kupima vyakula vya kila siku, vinavyowakilishwa na mafuta ya zeituni na divai ambavyo vilikuwa vyakula vya msingi nyakati hizo.
Tangu 1914 je, kuna mambo ya na horhi boyish a kwamba mpandaji wa farasi mweusi yuko mwendoni? Ndiyo! Ktk karne ya 20, watu wapatao milioni 70 walikufa kutokana na njaa.
Shirika moja lilikadiria kuwa " watu milioni 805, yaani, mtu mmoja kati ya watu tisa duniani kote hakupata chakula chenye lishe kati ya mwaka wa 2012 - 2014. Ripoti nyingine inasema hivi: " Kila mwaka, njaa huua watu wengi zaidi kuliko jumla ya watu wanaokufa kutokana na UKIMWI, malaria na kifua kikuu." Iicha ya jitihada nyingi za kuwalisha wenye njaa, mpandaji wa farasi mweusi bado anaendelea na mwendo
Asante sana rafiki tukutane juma lijalo hapa hapa msikivu blog asante sana
Maoni
Chapisha Maoni