Kichocho ni ugonjwa unaoshambulia mishipa ya kibofu cha mkojo au tumbo la chakula.
Dalili zake
Mtu hupata maumivu makali kwenye kibofu wakati wa kukojoa na maumivu makali ya tumbo anapoharisha.
Mtu hupungukiwa na damu
Mtu hukojoa damu au huharisha kinyesi chenye damu.
Mtu kuumwa tumbo mara kwa mara
Jinsi ya kujikinga
Tumia choo kwa haja kubwa na ndogo
Epuka kuogelea, kuoga, kunawa, kulima, kuvua, kucheza, kwenye maji yenye konokono wa kichocho
Tumia mazingira yanayozunguka nyumba za kuishi kwa kufyeka vichaka na kufukia madimbwi
Asante sana karibu juma lijalo hapa hapa msikivu blog
Maoni
Chapisha Maoni