Chungu wa rangivya fedha anayeishi katika jangwa la sahara ( cataglyphis bombycina ) Ni mmoja kati ya viumbe wenye uwezo mkubwa wa kuvumilia joto kali.
Wakati wa mchana eneo la sahara huwa na jua kali sana hivi kwamba wanyama ambao ni adui za chungu hutumia mwanya huo wa pekuu kutoka shimoni na kujitafutia chakula.
Kipindi hicho kinafaa kwani yeye hupata mizoga ya wadudu wengine waliokufa kutokana na joto kali
Jambo la kufikiria: Ngozi ya chungu wa rangivya fedha imefunikwa na vinyweleo vya pekee upande wa juu na pembeni, Lakini tumboni hakuna vinyweleo.
Vinyweleo ( 1, 2 ) ambavyo humfanya chungu huyo ang'ae, ni vyembamba na vina umbo la pembe tatu (3 ) pande mbili za vinyweleo hivyo zina matuta madogo madogo, wakati upande ule mwingine ni laini.
Muundo huu wa pekee hutimiza mambo mawili muhimu. Kwanza huwezesha vinyweleo kuakisi miali ya jua yenye joto. Pili, humwezesha chungu kutawanya joto la mwili wake.
Wakati huohuo, sehemu ya chini ya mwili wake isiyo na vinyweleo, huakisi joto la mchanga wa jangwa.
Ngozi ya chungu wa sahara ni kama mwavuli ambao humkinga na joto, na hivyo kudumisha kiwango cha joto ambacho anaweza kustahimili, yaani, chini ya nyuzi joto 53.6.
Kwa sababu ya kumchunguza mdudu huyo mdogo, watafiti wanajaribu kuunda njia ya pekee ambayo inaweza kutumiwa kupunguza joto bila kutumia feni.
Maoni
Chapisha Maoni