Kunawa uso ni miongoni mwa hatua muhimu ktk usafishaji wa eneo hilo.
Pamoja na kuwa watu wengi hususani wanawake, hutumia gipodozi mbalimbali kufanikisha jambo hili, yapo mambo kadhaa yanayopaswa kuzingatia ili kupata matokeo mazuri.
Mtandao wa beauttips.com umeainisha mambi hayo kuwa ni pamoja na
. Tumia vipodozi sahihi kwa ngozi yako. Uoshaji wa uso mara nyingi hutofautiana kulingana na aina ya ngozi lakini kwa ujumla wake huwa na lengo moja, nalo ni kuiacha ngozi ikiwa safi na yenye afya.
Watu wengi huamini kuwa matumizi ya sabuni zenye mapovu mengi huboresha zaidi ngozi zao, jambo linalopingwa na wataalamu wa ngozi.
Kikubwa unachotakiwa kuzingatia ni aina za kemikali zilizopo kwenye sabuni husika je zinaendana na ngozi yko?
. Tumia maji yenye hali joto sahihi Epuka kutumia maji yenye joto kali au baridi kali.
Kwani yanaweza kukusababbishua kuwa na tatizo la ukavu kwenye ngozi.
. Osha uso angalau mara mbili kwa siku kwenye maeneo ya baridi, lakini kama uko maeneo yenye joto fanya hivyo mara tatu na kumalizia kwa kupaka losheni.
Epuka kukaa juani hasa wakati wa jua kali.
. Epuka kujigusa usoni mara baada ya kusafisha uso wako
. Usitoe vipodozi kwa kunawa uso, badala yake tumie ' remover ' Hakikisha unafanya hivyo kabla ya kuosha ngozi yako ya uso
. Wakati mwingine unaweza kutumia vipidozi asilia ktk usafishaji wa uso wako. Ondoa ngozi zilizokufa, punguza mafuta yaliyoganda na pia lainisha ngozi yako kwa kutumia vipodozi asilia
Maoni
Chapisha Maoni