Zifuatazo nia alama zitakaokusaidia kuwa macho mara utakapoona mazingira ya kufanana nazo yanatokea ktk uhusiano wenu.
1 Anapenda kutembea na mipira ya kinga mara kwa mara ( kondomu )
Inashangaza mara nyingine kusikia mpenzi mmoja anatabia ya kubeba kondomu kwenye pichi yake au mfukoni kwa kisingizio kuwa anajali cha kushangaza zaidi unakuta yuko ktk mahusiano na mkewe au mumewe
2 Tabia ya kuficha fedha
Hii utaiona ghafla mpenzi wakeo anaanza kuwa na siri kuhusu fedha zake au matumizi yake, na wala hapendi kuulizwa ulizwa kuhusu suala hilo.
Tabia hii ikidhihirika ktk mapenzi yenu usichelewe kuchunguza maana kwa kukaa kimya uwnaweza kujikuta umechelea mwana na maji ya moto
3 kuzidi kwa tabia za kutoonekana au kuponyoka
Gafla siku hizi haagi anakwenda wapi, ukiuliza inawezakuwa vita.
Anakuwa na visa vya kumuwezesha kuponyoka
4 Harufu ambazo hujazizoea
Kwa kuwa wapendanao huwa wamezoeana, maranyingi hata aina ya manukato mmoja anayotumia yanakuwa yanajulikana kwa mwenzake, sasa embu fikiri unamkuta mpenzi wako ametokea na ana harufu tofauti
5 Tabia za kuanza kukufuatilia sana au hata kukuganda
Wapo wanaopeleka wapenzi wao kila wanakotaka, nakutoruhusu mazingira ya wapenzi hawa wakike kuwa huru kufanya mambo yao wenyewe, wengine waliitafsiri hali hii kama penzi kubwa lakini baada ya muda unagundua kuwa ile ilikuwa ni ujanja wa kuficha uhalisi wake na kuzuia mazingira kwa mpenzi wake kugundua au kupewa taarifa ta tabia zake.
Maoni
Chapisha Maoni