HARRY KANE _ Tottenham vs Apoel ( sept 26, 2017 )
Muingereza wa mwisho kabisa kupiga hat trick ktk Ligi ya Mabingwa wa ulaya.
Harry kane aliendeleza vipigo vya hat trick anavyotoa mwaka huu ktk pambano hilo dhidi ya Apoel ugenini na kuwa mchezaji wa saba wa kiingereza kupiga Hat trick ktk michuano hiyo
DANNY WELBECK - ARSENAL VS GALATASARAY ( OKT 1, 2014 )
Timu nyingine ya uturuki ambayo iliambulia makali ya mshmbuliaji wa kiingereza.
Ktk usiku huu wa Emirates, Gala walishindwa kabisa kumdhibiti Danny ambaye kipindi cha kwanza alifunga mara mbili akaongeza lingine kipindi cha pili
WAYNE ROONEY - MAN UNITED VS FENERBAHCE ( SEPT 28, 2004 )
Pambano la kwanza tu akiwa na jezi ya Manchester United baada ya kupiga hat trick dhidi ya Fenerbahce ya uturuki kwenye ligi ya mabingwa ulaya.
Mabao hayo yali tangaza jina lake.
Wengine ni Michael owen mwaka 22, okt 2002
Alan shearer mwaka 26, February 26, 2003 nk
Leo nimegusia bahazi ya waingereza walio piga hat trick ila wapo wengi waliofanya jambo hili.
Maoni
Chapisha Maoni