Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Mng'ao wa Bluu wa Beri Aina ya pollia

BERI ndogo aina ya Pollia condensata, inapatikana barani Afrika. Beri hii ina mwonekano wa bluu unaong'aa sana kuliko mmea mwingine wowote.

Hata hivyo basi, ni nini hufanya iwe na mng'ao wa bluu?

Fikiria: Chembe zilizo kwenye ngozi ya beri zina kuta zenye nyuzinyuzi nyembamba sana ambazo zimepangwa kama safu ya njiti za kiberiti.

Nyuzimyuzi hizo hufanyiza matabaka, kila tabaka likiwa limepinda kidogo ukilinganisha na la chini yake, na hivyo kufanyiza umbo la springi.

Nyuzinyuzi hizo hazina rangi ya bluubkwa sababu ya jinsi zilivyopangwa. Hivyo, kinachotokeza mwonekano wenye kung'aa, unaobadilika badilika si rangi bali ni mpangilio wa nyuzinyuzi.

Chembe nyingi huonekana kuwa za bluu. Lakini zinapotazamwa kutoka pande tofauti tofauti, zinaonekana kuwa za kijani, waridi, au njano ikitegemea matabaka hayo.

Kwa kuongezea, zinapochunguzwa kwa makini, beri hizo huonekana kuwa na madoadoa kama vile rangi kwenye skrini ya kompyuta.

Kwa sababu hazina rangi, beri hizo hazipotezi mng'ao wake wa bluu hata zina podondoka.

Wewe una maoni gani ? Je, mng'ao wa bluu wa beri aina ya pollia ulijitokeza wenyewe tu? Au ulibuniwa

Maoni

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

Utengenezaji wa sabuni

1: Utengenezaji wa sabuni za mche     Malighafi: 1: Caustic kg 4 2: Maji lita 10 3: Mafuta lita 20 4: Sodium Silicate Kg 2 5: pafyumu mili lita. 250 __  300 6: Chumvi vijiko 2 vikubwa Sabuni hii unaweza kuogea na kufulia inakuwa nzuri sana. Jinsi ya kutengeneza Loweka Caustic kg 4 kwenye maji ya lita 10 kwa siku 3. Ndani ya siku hizo tatu, utakuwa ukikoroga kila siku asubuhi na jioni kwa dakika 5. Kisha chukua sodium silicate kg2 ikifuatiwa na chumvi vijiko 2 vya chakula na mafuta huku unaendelea kukoroga kwa juhudi. Baada ya hapo weka kwenye maumbo kwa siku 3 __ 5 ili igande vizuri. Asante sana rafiki

Jinsi ya kutengeneza sabuni ya maji

Jinsi ya kutengeneza sabuni ya maji Malighafi: 1. Sulphonic Acid Lt 2 2. Soda Ash Kg 1 3. Sless Lt 1 4. Chumvi Kg 1 5. Pafyumu /rangi Bluu 6. Maji Lt 35 _ 40 Jinsi ya kutangeneza Anza kwa kuweka lita 10 mara tatu, yaani lita 10 tena na mwisho lita 10, angalia uzito ongeza tena lita 5 na kisha lita 2 ikiwa uzito bado ongeza lita 2 na mwisho lita 1 4. Chumvi kg 1 3. Sless Lt 1 2. Soda Ash Kg1 1. Sulphonics Acid Lt 2 Hapo sijaweka rangi wala pafyumu kwa sababu ukiweka pafyumu lita 35 bila kufunika itaisha baada ya muda mfupi. Ni vema rangi na pafyumu uweke pembeni. Mfano: Chukua ndoo ya lita 10, weka rangi robo kijiko cha chai na pafyumu vijiko vya chakula viwili na koroga vizuri. Ni vema utumie pafyumu aina ya lemon. Sababu za kutoweka rangi sabuni yote: Wapo wateja hawapendi rangi na harufu kwa hiyo utawapa kila mtu kama atakavyo na kujaza kwenye chupa zako zenye mifuniko saa hiyo hiyo ukiachia muda inatoka harufu. Asante sana rafiki.

Fahamu jinsi ya kutengeneza sabuni ya vyoo

Sabuni ya kusafisha vyoo Malighafi. 1. Sulphonics Acid Lita 1 2. Soda Ash nusu 1/2 kilo 3. Sless 4. Chumvi 1/2 kilo 5. Maji lita 17 1/2 _ 20 6. Rangi kijani 7. Pafyumu 8. Formalin Jinsi ya kutengeneza Weka maji lita 5 kisha anza kukoroga, ongeza lita 5 kisha lita 5 tena na mwisho lita 2 4. Chumvi 1/2 kg 3. Sless nusu lita 2. Soda ash nusu kilo 1. Sulphonics Acid lita 1 Hapo sijaweka rangi wala pafyumu ni vinzuri kuweka kwenye ndoo lita 10 ya sabuni utaweka rangi kijiko 1 cha chai, rangi ya kijani pafyumu aina ya ' Rose two one ' au pino vijiko 5 vya chakula na Formalin vijiko 3 vya chakula. Formalin kwa ajili ya kuua wadudu ( bacteria ) ni vinzuri sana kuwemo kwenye sabuni ya chooni kwani ina kazi nyingi zaidi ya hiyo iliyotajwa Asante sana rafiki sasa chukua hatua ya kufanya hakika utafanikiwa sana