Biblia inatushauri tudhibiti " tamaa ya macho " ( 1yohana2:15_17 ) matangazo yanaweza kuchochea tamaa hiyo, na hivyo kumsukuma mtu afanye kazi muda mrefu zaidi au kutafuta burudani zinazopita kiasi au zinazogharimu pesa nyingi.
Ni kweli kwamba huwezi kuepuka matangazo yote. Lakini unaweza kudhibiti kiasi cha matangazo unayoona na kusikia. Pia, chunguza kwa makini mambo ambayo unahitaji hasa.
Kumbuka pia kwamba watu unaoshirikiana nao wanaweza kukuathiri. Ikiwa wanatafuta kwa bidii vitu vya kimwili au wanapima mafanikio ya mtu kwa kutegemea mali zake, litakuwa jambo la hekima kutafuta narafiki wanaotanguliza mambo muhimu zaidi.
Biblia inasema " Anayetembea na watu wenye hekima atakuwa na hekima " methali 13:20.
Maoni
Chapisha Maoni