Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Viungo vya pango la mfupa wa nyonga ( the pelvic organs )

Ktk wanawake viungo vyenye maana kwa uzazi vyakaa ktk pango la mfupa wa nyonga, ndivyo: mji wa mimba ( uterus ) ulio katikati pamoja na mirija yake miwili ( tubes ) na kokwa mbili kwa kila upande. Mbele ya viungo hivi vya uzazi ni kibofu cha mkojo na upande wa nyuma ni mwisho wa utumbo mpana; havionekani nje.
Viungo hivi vimefunikwa na kitambi cha tumbo ( peritoneum ) Ngozi hiyo yatenga viungo vya pangoni na vile vya uvunguni mwa tumbo ( abdominal cavity )

Maoni