Nguo hutengenezwa kwa nyuzi zinazotoakana na utembo. Utembo huo hupatiakana kutoka kwa wanyama, mimea na mchanganyiko wa kemikali.
Utembo wa mimea hutupatia nguo za aina ya pamba na lineni. Utembo wa wanyama hutoa silki n sufu.
Utembo wa kemikali hutengenezwa nguo za utembo ni mashati, suruali, magauni, shuka, foronya, vyandarua, fulana na taulo.
Ufuaji nguo
Wakati wa kufua nguo ni muhimu kuwa waangalifu kwa sababu ya kuhifadhi muundo asilia wa nyuzi za nguo na vile vile rangi yake.
Hali kadhalika nguo hufuliwa kwa kuzingatia asili yake, iwapi ni nguo za pamba, sufu, silki, au nailoni.
Tendo la 1: kufua nguo nyeupe za pamba
Wakati wa kufua nguo za pamba lazima kuzingatia mambo muhimu kama vile tofauti ya nguo nyeupe za pamba au nguo za rangi.
Iwapo nguo ni nyeupe zifuliwe kama ifuatavyo.
Fua nguo hizo pekee bila ya kuzichanganya na nguo zo zote za rangi.
1. Loweka nguo kwa muda ili kulegeza uchafu.
2. Fua nguo hizo pekee bila ya kuzichanganya na nguo zo zote za rangi
3. Tumua sabuni yenye ditajenti kwa kuwa husaidia kung'ariaha nguo hizi
4. Chemsha kila inapolazimu, hasa zinapokuwa zimeanza kupoteza weupe wake
5. Suuza nguo vizuri na hakikisha sabuni imetoka vizuri
6. Tia bluu ktk nguo nyeupe kila inapolazimu
7. Anika nguo nyeupe za pamba juani baada ya kuzifua kwa sabuni, jua husaidia kuzitakasa, yaani kuzifanya nyeupe zaidi.
Tendo la 2: Kupiga pasi nguo nyeupe za pamba
Iwapo nguo zitapigwa pasi siku hiyo zianue kabla hazijakauka kbisa.
Zikunje kwa marefu yake kisha ziviringishe sana. Iwapi utazipiga pasi ktk siku inayofuata ziache juani kwenye kamba mpaka zikauke kabisa ndipi uzianue.
1. Nyunyuzia maji ktk nguo zilizokauka kabisa kisha ziviringishe ili unyevu uenee ktk nguo.
2. Tayarisha vifaa vyote vinavyotakiwa kwa kupuga pasi.
3. Anza kupiga pasi kwa ndani ktk sehemu zilizo maradufu kama vile, pindoni, kwenye sijafu na kwenye majongo. Sijafu ni pindo la ndani la mkono wa kanzu au koti.
4. Geuza nguo na piga pasi nguo yote ktk upande wa nje kwa kufuata nyuzi za matande.
5. Tandaza za nguo ziweze kupata hewa na kukauka sawasawa.
6. Kunja na weka sandukuni au kabatini.
Tendo la 3: Kufua nguo za nailoni
Nguo za namna hii mara nyingi ni imara na nyepesi. Haziruku wala haziharibiki umbo lake wakati wa kufuliwa.
Huweza kuyeyuka zikipata moto na kuweka makunyanzi ya kudumu zikipata joto kali.
1. Fua nguo ktk maji moto yenye povu la sabuni au ditajenti.
2. Fua kwa kufikicha nguo katikati ya mikono bila kusugua.
3. Suuza nguo ktk maji vuguvugu hadi povu litoke. Mwisho suuza ktk maji baridi.
4. Anika nguo bila kukamua iwapi ni za rangi anuwai. Zianike kivulini.
5. Nguo za nailoni hazipigwi pasi. Ikibidi kuzinyoosha tumia pasi yenye joto kidogo.
Asante sana
Maoni
Chapisha Maoni